Mcheza Tenis wa Uingereza Andy Murray amemshinda mchezaji mwenzake Novak Djokovic na kufanikiwa kushinda tuzo ya kwanza ya fainal za dunia za ATP 2016 akiwa kama mchezaji namba moja duniani.
Muray ameshinda fainal hizo kwa seti 6_3 na 6_4 katika uwanja wa 02 Arena mjini London.Murray mwenye miaka 29 amekuwa mchezaji bora katika mashindano 24.Murray aliyeshinda vikombe 34 kwa Mara kumi amesema "Ninayo furaha kubwa sana kuwa mshindi na kuwa namba moja Duniani ni kitu cha pekee sana alisema Murray.Nina furaha kabla ya hapa tumekuwa tukichuana katika fainal mbalimbali na katika Olimpiki lakini ninayo furaha kubwa kuwa Mshindi alisema Murray.