Tino Ze Mastermind: March 2017

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

NAY WA MITEGO ADAI KUKAMATWA NA POLISI MVOMERO NI KUTOKANA NA WIMBO WAKE "WAPO" UNAIKOSOA SERIKALI.

Msanii wa bongo flava Ney wa Mitego amedai kukamatwa na polisi wilayani mvomero morogoro alikokuwa amekwenda kwa ajili ya show.Hajaxema sababu ya kukamatwa kwake lakini watu wanahisi ni kutokana na wimbo wake "wapo" ambao umemkosoa vikali rais Dk John Magufuli.


Kupitia akaunti ya Instagram rapa ney wa mitego ameandika "nimekamatwa kweli muda huu nikiwa hotel Morogoro baada ya kumaliza kazi yangu iliyonileta napelekwa mvomero police nawapenda Watanzania wote #Truth #Wapo "alimalizia msanii huyo.

Hata hivyo kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro Ulrich Mtei ameongea na kusema "ni kweli huyu bwana anashikiliwa na polisi morogoro na shauri lake si la morogoro,tulipata tu maelezo kwamba tumtafute"alimalizia Kamanda Ulrich Mtei.

Magazeti ya Leo Jumapili Tanzania March 26

Hizi hapa kurasa za magazeti ya Leo Jumapili kuanzia Habari za Siasa Jamii Dini na Michezo.

MBWANA SAMATTA AFANYA KUFURU MBELE YA NAPE NA MWAKYEMBE.

Nahodha wa timu ya Taifa stars Mbwana Samatta ametupia magoli 2 kwenye mchezo dhidi ya Botswana katika dk 2 na 88.


Mbwana Samatta ametimiza ahadi yake kwa Watanzania ambayo aliahidi kabla ya mchezo mapema juzi alivyokuwa akizungumza na waandishi wa habari.


Katika Mchezo huo uliofanyika uwanja wa taifa waziri mpya wa Habari Sanaa na Utamaduni  Harson Mwakyembe alihudhuria kwenye mchezo huo akiwa na aliyekuwa waziri wa Wizara hiyo Nape Nnauye.

ALIYEMTOLEA BASTOLA MBUNGE NAPE NNAUYE MATATANI.

Jeshi la Polisi limesema limeanza kufanyia kazi maagizo waliyopatiwa na waziri wa mambo ya ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba kumsaka mtu aliyemtolea bastora aliyekuwa waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo Nape Nnauye.



Hayo yalisemwa Jana na msemaji wa jeshi la Polisi Advera Senso"sisi tumepokea maelezo ya Waziri na tayari tumeanza kuyafanyia kazi hilo ndilo ninaloweza kukwambia alimaliza msemaji huyo wa Polisi.Juzi waziri Mwigulu Nchemba alitoa taarifa na kusema "nahusika na usalama wa raia wote wa Tanzania nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kwa kofia ya Uaskari na kama askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika zichukue mkondo wake.