Jeshi la Polisi limesema limeanza kufanyia kazi maagizo waliyopatiwa na waziri wa mambo ya ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba kumsaka mtu aliyemtolea bastora aliyekuwa waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo Nape Nnauye.
Hayo yalisemwa Jana na msemaji wa jeshi la Polisi Advera Senso"sisi tumepokea maelezo ya Waziri na tayari tumeanza kuyafanyia kazi hilo ndilo ninaloweza kukwambia alimaliza msemaji huyo wa Polisi.Juzi waziri Mwigulu Nchemba alitoa taarifa na kusema "nahusika na usalama wa raia wote wa Tanzania nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kwa kofia ya Uaskari na kama askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika zichukue mkondo wake.