Msanii wa bongo flava Ney wa Mitego amedai kukamatwa na polisi wilayani mvomero morogoro alikokuwa amekwenda kwa ajili ya show.Hajaxema sababu ya kukamatwa kwake lakini watu wanahisi ni kutokana na wimbo wake "wapo" ambao umemkosoa vikali rais Dk John Magufuli.
Kupitia akaunti ya Instagram rapa ney wa mitego ameandika "nimekamatwa kweli muda huu nikiwa hotel Morogoro baada ya kumaliza kazi yangu iliyonileta napelekwa mvomero police nawapenda Watanzania wote #Truth #Wapo "alimalizia msanii huyo.
Hata hivyo kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro Ulrich Mtei ameongea na kusema "ni kweli huyu bwana anashikiliwa na polisi morogoro na shauri lake si la morogoro,tulipata tu maelezo kwamba tumtafute"alimalizia Kamanda Ulrich Mtei.