PICHA : TANZIA : SHABIKI WA SUNDERLAND BRADLEY LOWERY ALIYEGUSA NYOYO ZA WENGI AFARIKI DUNIA.
Shabiki wa klabu ya Sunderland wa umri wa miaka sita Bradley Lowery, ambaye tatizo lake la kiafya liligusa nyoyo za wengi amefariki dunia.
Bradley alikuwa anaugua ugonjwa ambao wa Kiingereza hufahamika kama neuroblastoma - aina nadra ya saratani - tangu alipokuwa na umri wa miezi 18. Bradley alifanywa kuwa shabiki -nembo ya klabu hiyo na akaunda urafiki wa karibu na mshambuliaji wa klabu hiyo Jermain Defoe.
Aidha, aliongoza wachezaji wa England kuingia uwanjani Wembley wakati wa mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Lithuania. Kifo chake kimethibitishwa na wazazi wake kwenye mitandao ya kijamii.
"Kijana wetu mkakamavu ameenda kuwa na malaika leo. "Alikuwa shujaa wetu na alipigana sana lakini alihitajika kwingine. Hatuna maneno ya kueleza jinsi tulivyohuzunishwa na kifo chake." Mamayake Bradley Gemma Lowery alikuwa akilia amesema mvulana huyo alikuwa amedhoofika sana Bradley alipewa matibabu lakini saratani yake ikaibuka tena mwaka jana.
Wahisani walichangisha zaidi ya £700,000 kulipia matibabu yake New York mwaka 2016, lakini madaktari waligundua kwamba saratani yake ilikuwa imeenea sana na hangeweza kutibiwa. Wazazi wake Gemma na Carl, kutoka Blackhall Colliery, Durham, waliambia Desemba kwamba alikuwa amesalia na "miezi kadha tu ya kuishi".
Miezi minne baadaye, walifahamishwa kwamba jaribio la mwisho kabisa la kumtibu lilikuwa limefeli. Bradley aliipenda sana Sunderland AFC na alikaribishwa uwanjani Stadium of Light.
Bradley Lowery alipendwa na maelfu ya watu na alipokea kadi 250,000 za kumtakia heri wakati wa Krismasi, kutoka kwa watu mataifa ya mbali kama vile Australia na New Zealand.
TUTAKUMBUKA DAIMA BRADLEY.
SAFARI YA ROMELU LUKAKU YAIVA KUTUA MIKONONI MWA MOURINHO.
Manchester United wameafikiana na klabu ya Everton kulipa £75m kumchukua mshambuliaji Romelu Lukaku ambapo usiku wa Alhamisi hii anadaiwa kupelekwa Los Angeles Marekani, kwaajili ya kufanyiwa vipimo ili kukamilisha deal hilo.
Mazungumzo kuhusu kuhama kwa Lukaku hayahusiani na mazungumzo kuhusu uwezekano wa mshambuliaji wa United Wayne Rooney kurejea Everton. Klabu hiyo ya Jose Mourinho ina matumaini kwamba itakamilisha usajili wa Lukaku kwa wakati kumuwezesha kujiunga na kikosi cha timu hiyo kitakachosafiri kucheza mechi za kabla ya msimu nchini Marekani Jumapili.
Mshambuliaji huyo alikuwa miongoni mwa orodha ya wachezaji ambao Mourinho aliwasilisha kwa naibu mwenyekiti wa klabu hiyo Ed Woodward kwamba alitaka kuwanunua kabla ya msimu kumalizika.
Awali, ilidhaniwa Lukaku angerejea katika kalbu yake ya awali Chelsea, ambayo alijiunga nayo kutoka Anderlecht mwaka 2011. Mshambuliaji huyo aliuziwa Everton kwa £28m na Mourinho mkufunzi huyo kutoka Ureno alipokuwa katika kipindi chake cha ukufunzi Chelsea mwaka 2014.
Lukaku ni mteja wa wakala Mino Raiola, ambaye pia huwasimamia Paul Pogba, Zlatan Ibrahimovic na Henrikh Mkhitaryan – wachezaji watatu walionunuliwa na United majira ya joto msimu uliopita.
Mbelgiji huyo alikataa ofa ya juu sana kutoka Everton Machi na kusema: “Sitaki kusalia katika kiwango sawa. Ninataka kujiboresha na najua ni wapi nahitaji kwenda out in is a hilo.”
PICHA : OMMY DIMPOZ RASMI ASAINI ROCK STAR 4000
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ommy Dimpoz amesaini kufanya kazi na label kubwa ya muziki, RockStar4000 inayofanya kazi kwa ukaribu na kampuni kubwa ya muziki duniani, Sony Music Entertainment.
Ommy Dimpoz amesaini RockStar 4000 hivyo kwa sasa ataungana na Alikiba ambaye alijiunga na label hiyo miaka 6 iliyopita, ambapo wiki iliyopita alitangazwa kuwa mmoja kati ya wamiliki wa label hiyo.
“Tanzanian Superstar singer-songwriter Ommy Dimpoz signed global exclusive management deal with #ROCKSTAR4000 & content deal #RockstarTV at the Rockstar Pan Africa Group HQ in South Africa,” ilisema taarifa hiyo ya RockStar4000.
Baada ya taarifa hiyo muimbaji huyo alizungumzia kuhusu deal hiyo. “Ni kweli nimesaini RockStar4000 kama ulivyosikia, kwahiyo kwa sasa nitakuwa nafanya kazi au kwa kifupi kazi zangu kuanzia sasa zitakuwa chini ya RockStar4000,” alisema Ommy Dimpoz. “Nilikaa nao chini tukazungumza nikaona hili ni jambo zuri kwangu kwa sababu RockStar4000 ni kampuni kubwa duniani ambayo inafanya kazi za wasanii wengi sana".
"Kwahiyo PKP ikaona bora tufanye nao kazi ili kuupeleka muziki wa Ommy Dimpoz mbali zaidi. Kwahiyo mashabiki wakae mkao wa kula kwaajili ya Ommy mwingine ambaye atakuwa na sura nyingine kabisa,” aliongeza Ommy Dimpoz.
Pia label hiyo nchini Tanzania inafanya kazi na muimbaji Lady Jay Dee pamoja na Baraka The Prince.