Gemma, ambaye ni mama mzazi wa Bradley Lowery (6), ametoa taarifa ya familia kuhusu kuendelea kuzorota kwa afya ya mtoto wao ambaye kwa muda mrefu amekuwa anasumbuliwa na kansa aina ambayo haiponyenyeki.
"Bradley amedhoofu sana na kwa uchungu mkubwa tunamwona anavyopigania uhai wake bila kujua namna nyingine ya kumsaidia; amekuwa anapumua kwa tabu sana. Kila jambo tumeendelea kumwachia Mungu," amesema Mama Bradley.
Ikiwa kama ishara ya kutaka kuonana kwa mara ya mwisho na watu wake wa karibu, Bradley aliwaomba wazazi wake wawaite marafiki zake mchezaji Jermaine's Defao na marafiki zake wengine wa umri wake ili aweze kuongea yake..
Jermaine Defoe (34) alifika hospitalini hapo na kutumia muda mrefu akiwa anaongea mambo mbali mbali ya kumtia moyo rafikiye Bradley hadi mtoto akalala kfuani mwa mchezaji huyo. Hali hii na upendo wa Defoe uliwaliza wengi hapo hospitali kwani namna Bradley alivyomkumbatia Jermaine akilala amelala ni kama aliyekuwa anamuaga.
Bradley alisema "huu ni wakati mgumu sana katika maisha yangu. Bradley ni mfano wa kuigwa kuhusu namna tunavyopaswa kupambana. Ninamwomba Mungu akipenda abadili matokeo nisitoyataka yamtokee Bradley."