PICHA : OMMY DIMPOZ RASMI ASAINI ROCK STAR 4000 | Tino Ze Mastermind

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

PICHA : OMMY DIMPOZ RASMI ASAINI ROCK STAR 4000

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ommy Dimpoz amesaini kufanya kazi na label kubwa ya muziki, RockStar4000 inayofanya kazi kwa ukaribu na kampuni kubwa ya muziki duniani, Sony Music Entertainment.

Ommy Dimpoz amesaini RockStar 4000 hivyo kwa sasa ataungana na Alikiba ambaye alijiunga na label hiyo miaka 6 iliyopita, ambapo wiki iliyopita alitangazwa kuwa mmoja kati ya wamiliki wa label hiyo.

“Tanzanian Superstar singer-songwriter Ommy Dimpoz signed global exclusive management deal with #ROCKSTAR4000 & content deal #RockstarTV at the Rockstar Pan Africa Group HQ in South Africa,” ilisema taarifa hiyo ya RockStar4000.

Baada ya taarifa hiyo  muimbaji huyo alizungumzia kuhusu deal hiyo. “Ni kweli nimesaini RockStar4000 kama ulivyosikia, kwahiyo kwa sasa nitakuwa nafanya kazi au kwa kifupi kazi zangu kuanzia sasa zitakuwa chini ya RockStar4000,” alisema Ommy Dimpoz. “Nilikaa nao chini tukazungumza nikaona hili ni jambo zuri kwangu kwa sababu RockStar4000 ni kampuni kubwa duniani ambayo inafanya kazi za wasanii wengi sana".

"Kwahiyo PKP ikaona bora tufanye nao kazi ili kuupeleka muziki wa Ommy Dimpoz mbali zaidi. Kwahiyo mashabiki wakae mkao wa kula kwaajili ya Ommy mwingine ambaye atakuwa na sura nyingine kabisa,” aliongeza Ommy Dimpoz.

Pia label hiyo nchini Tanzania inafanya kazi na muimbaji Lady Jay Dee pamoja na Baraka The Prince.

SHARE HABARI HII NA WENZAKO WAIPATE
KAMA UKIHITAJI KUWEKEWA MUONEKANO MZURI(BLOG DESIGNING) WA BLOG YAKO KAMA HUU WASILIANA NA RUBEN EMMANUEL KWA NAMBA 0716528779/0755542721 KARIBU SANA

google+

linkedin

About Author
  • ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More