Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Argentina na Klabu ya Barcelona Lionel Messi amemuoa mpenzi wake wa siku nyingi Antonela Roccuzo hapo jana katika hoteli ya kifahali ya Rosaria nchini Argentina.
Messi mwenye umri wa miaka 30 na mkewe Antonela Rocuzzo miaka 29 wamekuwa wapenzi tangu utotoni na huku familia zao zikiwa zimeishi karibu karibu.
Harusi hiyo ya Mchezaji huyo bora duniani ilikuwa na wageni waalikwa 260 pekee huku maelfu ya askari Polisi wakitanda maeneo hayo ya Harusi ilipofanyika.
Messi alikutana na Rocuzzo akiwa na umri wa miaka 13 kabla ya kuhamia Hispania.Miongoni mwa wageni waalikwa hapo Jana siku ya Ijumaa ni Pamoja na Luis Suarez,Neymar,Gerald Pigue akiwa na mkewe Shakira.Wageni wengi waliwasili na ndege binafsi, Magazeti ya Nchini Argentina yameandika hii ni Harusi ya Mwaka.
Hizi hapa ni Picha za harusi hiyo: