Msanii Nedy Muziki anayefanya poa na ngoma yake "Doze"amejibu kauli ya Dogo Janja anayexema hajui kuvaa amesema Dogo huyo hana Adabu kwa watu wazima ndio maana ametoa kauli hiyo kwake ambaye ni kaka yake kwenye mitupio.
Nedy ametoa jibu hilo kwenye kipindi cha 5Selekt cha EATV kwa kusema kwamba Dogo janja kumfananisha na Mkongo kwenye suala la kuvaa ni kukosa adabu ndio maana hata alipojua amekosea akaanza kujitetea kwamba watu wanawapambanisha.
"Dogo Janja hana heshima ndiyo maana aliweza kuzungumza kauli ile, Naweza kumfananisha na kijana anayeweza kuwakuta wazee wamekaa bila kusalimia alafu akauliza mbona hamjanisalimia wakati ni wajibu wake kuanza kuwasalimia . Sasa Janjaro ni mdogo wangu kwenye suala la mavazi. Mtu ambaye anawaza kukaa chini na kunipambanisha naye atakuwa ana matatizo ya akili na achunguzwe vizuri" - Neddy Music.
Pamoja na hayo Neddy ameweka wazi kwamba hana Matatizo yoyote na msanii huyo ambaye kwa sasa anasumbua masikio ya mashabiki zake inayokwenda kwa jina la 'Ukivaaje unapendeza' ndiyo maana hakutaka kubishana naye au kutengeneza bifu.
NEDDY : DOGO JANJA HANA ADABU.
IGP SIRRO Atangaza Dau nono kwa atakayetoa Taarifa ya Mauaji Kibiti.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Simon Sirro, avalia njuga matukio ya uhalifu yanayoweka rehani amani ya nchini.
Awali IGP Sirro ametuma Salamu za kwa wahalifu na kuwapa neno la faraja Wananchi wa Kibiti , Ikwiriri pamoja na Mkuranga na Rufiji.
IGP Sirro amekula kipao mbele ya suala la Mauji ya Raia kibiti na kuweka Dau kwa Wananchi watakao waonyesha wauaji wa Raia.
Ameweka mikakati ya kutokomeza uhalifu huo kwa kuanza kuongeza nguvu ya ziada kukabiriana na uhalifu huo.
Suala la Pili la ni Rushwa kwa Askari wa Jeshi la Polisi na kwamba askari au mtumishi wa jeshi hilo akicjihusisha na Rushwa atachukuliwa hatua za kisheria.
Suala la Mwisho ni kwamba kukomesha mauji yanayotokana na wananchi kujichukulia sheria Mkononi (watu wenye asira kali) na kwamba watachukuliwa hatua Kali.
MAZISHI YA IVAN : WATOTO WA MAREHEMU WATOA UJUMBE WA MWISHO MATAJIRI WAMWAGA PESA KWENYE KABURI.
Shughuli ya kuuzika mwili wa mfanyabiashara maarufu nchini Uganda na Afrika Kusini ambaye pia alikuwa mume wa Zarina Hassan, Ivan Ssemwaga zinaendelea katika makaburi ya ukoo wake yaliyoko Kayunga, nchini Uganda.
Zari akiwa na watoto wake mbele ya jeneza
Baada ya jana Zari kutoka kauli yake ya kwanza toka Ivan kufariki, Leo watoto wa marehemu wametoa kauli yao ya mwisho kwa marehemu baba yao.
Soma taarifa hii…
“Dad, so many thoughts come to our mind whenever we speak of your name; it seems without you in our lives things will never be the same. We think of the good old days when we were still so little; consumed in your love, and in your smile.”
“Those days are gone and no matter what we do, life will never be the same! Oh Dad, if only we could turn back the hands of time and hear your voice once more, but God called you to a better place, so peaceful and free of pain. And when we see you sleeping, we can only wish the best for you.”
Ivan Semwanga alifariki katika Hospitali ya Biko Academy nchini Afrika Kusini, Alhamisi wiki iliyopita kutokana na ugonjwa wa moyo na anazikwa leo.