Majeruhi wa Lucky Vicent Wanaotibiwa Marekani Mmoja atoka Nje kwa Mara Ya Kwanza. | Tino Ze Mastermind

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Majeruhi wa Lucky Vicent Wanaotibiwa Marekani Mmoja atoka Nje kwa Mara Ya Kwanza.

Majeruhi wa ajali ya Basi la wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent waliopelekwa nchini Marekani imeripotiwa hali zao kuendelea vizuri huku mmoja kati yao Wilson kwa Mara ya Kwanza ametoka nje.

Mtoto Wilson akiwa kwenye "wheel chair"huku mama yake na Daktari wake wakiwa kwenye Tabasamu mara baada ya kutoka nje ya jengo la Hospital.


Taarifa iliyotolewa na Mbunge wa Singida Kaskazini Mh Lazaro Nyalandu imeeleza kuwa mtoto Doreen amemaliza kufanyiwa upasuaji wa Uti wa Mgongo kwa kile ambacho Madaktari wamesema wamefanikiwa kwa Ufanisi Mkubwa kupita matarajio yao.

Doreen alikuwa afanyiwe upasuaji kwa makadirio ya Masaa 5.30 lakini zoezi hili lilikamilika kwa mda wa Masaa 4 huku timu ya "Surgical "ikiwa na watu sita na kwa Pamoja wakiongozwa na Madaktari Bingwa wawili Dr. Meyer na Dr. Durward.

Doreen amehamishwa katika chumba cha Upasuaji na kupelekwa ICU ambako wamempumzisha baada ya upasuaji na kumrudisha wodi ya watoto ambako ataendelea na mapumziko.Mungu amesikia maombi ya Watanzania na wote waliotoa Sala zao kwa ajili ya mtoto Doreen popote Duniani.

Doreen Mara baada ya Upasuaji.
SHARE HABARI HII NA WENZAKO WAIPATE
KAMA UKIHITAJI KUWEKEWA MUONEKANO MZURI(BLOG DESIGNING) WA BLOG YAKO KAMA HUU WASILIANA NA RUBEN EMMANUEL KWA NAMBA 0716528779/0755542721 KARIBU SANA

google+

linkedin

About Author
  • ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More