Msanii Nedy Muziki anayefanya poa na ngoma yake "Doze"amejibu kauli ya Dogo Janja anayexema hajui kuvaa amesema Dogo huyo hana Adabu kwa watu wazima ndio maana ametoa kauli hiyo kwake ambaye ni kaka yake kwenye mitupio.
Nedy ametoa jibu hilo kwenye kipindi cha 5Selekt cha EATV kwa kusema kwamba Dogo janja kumfananisha na Mkongo kwenye suala la kuvaa ni kukosa adabu ndio maana hata alipojua amekosea akaanza kujitetea kwamba watu wanawapambanisha.
"Dogo Janja hana heshima ndiyo maana aliweza kuzungumza kauli ile, Naweza kumfananisha na kijana anayeweza kuwakuta wazee wamekaa bila kusalimia alafu akauliza mbona hamjanisalimia wakati ni wajibu wake kuanza kuwasalimia . Sasa Janjaro ni mdogo wangu kwenye suala la mavazi. Mtu ambaye anawaza kukaa chini na kunipambanisha naye atakuwa ana matatizo ya akili na achunguzwe vizuri" - Neddy Music.
Pamoja na hayo Neddy ameweka wazi kwamba hana Matatizo yoyote na msanii huyo ambaye kwa sasa anasumbua masikio ya mashabiki zake inayokwenda kwa jina la 'Ukivaaje unapendeza' ndiyo maana hakutaka kubishana naye au kutengeneza bifu.
NEDDY : DOGO JANJA HANA ADABU.
Published Under
ENTERTAINMENT
About Author
ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More