IVAN KUZIKWA LEO : ZARI AAHIDI KUWAANGALIA WATOTO
Published Under
ENTERTAINMENT
Baada ya Jumatatu hii mwili wa Ivan Ssemwanga kuagwa na kufanyiwa ibada takatifu, aliyekuwa mke wa zamani wa marehemu, Zari Hassan alipata fursa ya kuzungumza kwa mara ya kwanza.
Katika misa ya mazishi iliyofanyika kwenye kanisa la Namirembe mijini Kampala, Uganda Jumatatu hii, Zari alionekana akiwa ametulia na akizungumza na wanae.
Alipoitwa kuzungumza madhabahuni, watu waliohudhuria walijianda kumsikiliza atakachosema.
“Sitomhuzunikia Ivan,” alisema. “Nitasherehekea maisha yake. Muda mrefu, tulitengana kwasababu ya tofauti ambazo sote tulizijua. Nilisonga mbele na maisha yangu, lakini si Ivan. Ivan alijua kile nilichoweza kufanya. Alijua kile nilichoweza kufanya na kile nisichoweza. Alijua kuwa ningewaangalia vijana vyema na aliniamini. Kwa hali hiyo, naahidi ntawaangalia vijana hadi nitakapoungana naye.”
Ivan anatarajiwa kuzikwa leo ambapo Diamond aliyezaa na Zari watoto wawili naye aliahidi atahudhuria.SHARE HABARI HII NA WENZAKO WAIPATE KAMA UKIHITAJI KUWEKEWA MUONEKANO MZURI(BLOG DESIGNING) WA BLOG YAKO KAMA HUU WASILIANA NA RUBEN EMMANUEL KWA NAMBA 0716528779/0755542721 KARIBU SANA
About Author
ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More