Hatimaye timu ya Yanga imeweza kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2016/2017 ukiwa ni ubingwa wa 3 mfululizo na kufikia jumla ya vikombe 27 vya Ligi kuu Tanzania Bara.
Ingawa Timu ya Yanga walikubali kipigo cha 2 mfululizo dhidi ya Mbao FC kwa kufungwa goli 1_0 wamewazidi timu ya Simba kwa tofauti Ya Magoli.
Timu zilizoshuka daraja la ligi kuu ya Tanzania Bara ni African Lyon,Toto African na Jkt Ruvu.
Haya hapa matokeo ya Timu nyingine zilizochezwa Leo na kukamilisha Ligi kuu ya Vodacom Premier League msimu wa 2016/2017.