Mchezaji wa Manchester United Ibrahimovic ameshinda tuzo ya Mchezaji bora wa EPL mwezi disemba.Kwa upande wa kocha wa Chelsea Antonie Conte ameshinda tuzo ya kocha bora wa EPL mwezi Disemba.
IBRAHIMOVIC, MKHITARYAN NA CONTE WASHINDA TUZO ZA EPL.
Published Under
M I CH E Z O
Kwa upande wa Kocha wa Chelsea Antonie Conte hii ni mara ya 3 mfululizo Muitalia huyu kubeba tuzo hiyo.
Mchezaji wa klabu ya Manchester United
ambaye ni raia wa Armenia Henrikh Mkhitarayan baada ya kufunga bao ambalo lilikuwa gumzo ambalo lilipewa jina la goli la "Scorpion" ameshinda tuzo ya goli bora la mwezi Disemba.
SHARE!
PICHA : ANGALIA PICHA ZA JENNIFER NA PATRICK WA KANUMBA WALIVYOKUWA WAKUBWA.
Published Under
ENTERTAINMENT
Huwenda ukikutana barabarani na Hanifa Daud "Jennifer" pamoja na Othman Njaidi "Patrick" ambao ni zao la marehemu Steven Kanumba na usiweze kuwafahamu kwa jinsi walivyokuwa wakubwa.
Vijana hao wawili walifanya vizuri ndani ya filamu za Uncle JJ pamoja na This is It wakiwa na marehemu Steven Kanumba.
Jennifer ambaye mwaka 2016 alionekana kwenye filamu ya Zena na Betina ya Salma Jabu "Nisha" amehitimu kidato cha 4 mwaka huu.Kwa upande wa
Patrick 2016 alihojiwa na mtandao mmoja wa Habari na kudai hana mzuka wa kuigiza kwa sasa kama zamani.Hizi hapa Picha zao walivyo sasa :
SHARE!
MAHREZ ASHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA 2016 HII HAPA ORODHA YA WASHINDI WOTE.
Published Under
M I CH E Z O
Shirikisho la soka Afrika CAF usiku wa kuamkia Leo limetoa Tuzo kwa wachezaji,timu na waamuzi waliofanya vizuri katika sekta hiyo ya Michezo kwa mwaka 2016.
Hafla hiyo iliyofanyika nchini Nigeria ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Soka lakini pia ikiwa imepambwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali ikiwemo Diamond Platnumz na Rayvanny kutoka Nchini Tanzania.
Wachezaji na timu mbalimbali zilitajwa kuwania tuzo hizo katika vipengele tofauti.Hii hapa chini Orodha ya washindi katika vipengele mbalimbali :
1.Tuzo ya timu bora ya Taifa ya Wanawake ilikwenda kwa Timu ya Nigeria Super Falcons baada ya kutwaa kombe la Afcon kwa mara ya 8.
2.Tuzo ya klabu bora ilikwenda kwa Mamelodi Sundowns Fc ya South Africa baada ya kutwaa kombe la klabu Bingwa Afrika.
3.Kocha bora wa mwaka 2016 ni Pitso Mosimane kutoka Afrika kusini.
4.Tuzo ya Most Promising Talent ilikwenda kwa Kelechi Ihenacho kutoka Nigeria anayeichezea Man City.
5.Mchezaji bora wa kike ni Asisat Oshoala kutoka Nigeria anayekipiga katika klabu ya wanawake ya Arsenal.
6.Mwamuzi bora ni Bakary Papa Gassama kutoka nchini Gambia.
7.Timu bora ya Taifa ya Wanaume ni timu ya Taifa ya Uganda The Cranes.
8.kikosi bora cha mwaka 2016.
9.Mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani ni Denis Onyango kutoka Uganda na klabu ya Mamelodi Sundowns.
10.Mchezaji bora wa Afrika ni Riyad Mahrez kutoka Algeria anayekipiga katika klabu ya Leicester City ya Uingereza.
SHARE!
Ajinyonga Hadi Kufa Baada Ya Mkewe Kumnyima Samaki.
Published Under
MATUKIO
Mkazi mmoja wa kijiji cha Kalunde kilichopo Kata ya Kipande wilayani Nkasi Vedasti Kazumba 51 amejiua kwa kujinyonga kwa kile kinachodaiwa kuwa alighadhabika baada ya Mkewe kumnyima kitoweo cha Samaki.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa George Kyando alithibitisha tukio hilo na kusema lilitokea usiku wa mkesha wa mwaka mpya na kwamba Kazumba alifikia uamuzi huo mgumu kwa kujinyonga akitumia kamba ya Katani.
Alieleza hakuna mtu anayeshikiliwa na Polisi kuhusu tukio hilo na Uchunguzi wake unaendelea.
Habari kutoka kijijini humo kinaeleza kuwa chanzo cha Kazumba kujinyonga ni kukasirishwa na kitendo cha mkewe Antoniata Mwisua kumnyima kitoweo cha Samaki.
"Mke wa marehemu aitwae Antoniata alimwandalia mumewe huyo chakula cha Usiku kitoweo chake kikiwa ni Samaki mbichi Alimkomba samaki huyo kisha akamwomba amwongezee kitoweo kingine cha Samaki,lakini mkewe alimweleza kitoweo kimekwisha ndipo mumewe alipokasirika akidai kuwa
Mkewe amemnyima kwa makusudi kitoweo hicho ndipo alipochukua hatua ya kuzira kula" alieleza mmoja wa mashuhuda kwa masharti ya kutotajwa.
Mwenyekiti wa kijiji cha Kalunde John Kalasa alidai kuwa marehemu wakati wa Uhai wake alikuwa ni mtu mwenye kujawa na Ghadhabu ambapo Mara kadhaa alisikika akitishia kujinyonga.
SHARE!
Subscribe to:
Posts (Atom)