Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Patrick Malindisa 29 mkazi wa mtaa wa Namanyigu Kata ya Mshangano Manis ya Songea mkoani humo kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi Atanasi Malindisa 70 kwa kumpiga na kitu chenya Ncha butu kichwani na kidevuni upande wa kushoto na kisha kufanya jaribio la kuchimba shimo kwenye nyumba hiyo kwa malengo ya kumzika baba huyo.
Akizungumza katika eneo la tukio mmoja wa wanafamilia ambaye ni mdogo wa marehemu Pius Malindisa alisema kuwa wao walipata taarifa ya kifo cha ndugu yao Januari 1 kutoka kwa mtoto wa marehemi Patrick Malindisa.
Pius alisema kuwa mtoto huyo ambaye alikuwa akiishi kwenye nyumba hiyo na marehemu alitoa taarifa kwa wanandugu
"Kuwa baba yake amefariki kwa homa ya tumbo na ndugu walipofika kabla ya kuingia chumbani alikokuwa akilala marehemu waliamua kuita uongozi wa mtaa ambao uliingia na kubaini kuwa Marehemu ameuawa kwa kupigwa na kitu kichwani na kidevuni.
"Tulipofika hapa tulikuta shimo limechimbwa ndani ya nyumba na inaelekea lilimshinda na kuamua kuanza kutoa taarifa kwetu ambapo alidai alikuwa anaumwa ugonjwa wa Tumbo"alisema Pius.
Alisema kuwa baada ya kubaini hilo walitoa taarifa Polisi kisha mwili kuchukuliwa na kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma (HOMSO)
Kwa uchunguzi huku jeshi la Polisi likimshikilia mtoto wa Marehemu.