Mwigizaji wa Bongo movie Jacquelin Wolper ametumia mtandao wa Instagram kuonesha kitu gani kinaendelea kati yake na Harmonize.
Usisahau Jacquelin Wolper na Harmonize aka "woha'ama vyovyote ulivyokuwa ukiwaita pamoja.
Wolper amembwaga rasmi hitmaker huyo wa Bado Harmonize kupitia mtandao wa Instagram aliweka Post haikuweza kukaa kwa muda mrefu akaifuta japo wapo waliowahi kuinasa mapema.
Kwenye Post hiyo iliyokuwa na emoji za alama za kopa iliyopasuka wolper aliandika "Nina akili timamu me siyo mtoto mdogo, endelea na maisha yako it over waambie rasmi usifiche @harmonize_tz I hate love" alimalizia Wolper.
Inaonekana Harmonize kauvunja moyo wa Wolper kiasi cha kuyachukia Mapenzi kiasi hicho.