Staa wa bongo Flava Diamond Platnumz SIMBA na msanii wake Rayvanny wanatarajiwa kutumbuiza alhamisi hii tarehe 5 kwenye tuzo za Shirikisho la soka Barani Africa CAF zitakazotolewa mjini Abuja Nigeria.
Wawili hao watatumbuiza wimbo wa "Salome" uliokuwa wa pili kwa ukubwa Afrika mwaka Jana baada ya Pana ya Tekno.Kupitia mtandao wake wa Instagram Diamond ameandika "Glo caf awards rehearsal na Vanny bway!!! Tomorrow will be Performing your favorite song #Salome na @rayvanny.
Naye Rayvanny ameshare Picha kadhaa akiwa kwenye ukumbi zitakapotolewa tuzo hizo akifanya rehearsal na bosi wake.Pia ameshare video akizungumza na Mastaa wengine watakaotumbuiza kwenye tuzo hizo akiwemo Yemi alade na Mr Flavour.
Wasanii wa Afrika kusini Muffinz nao watatumbuiza.Pia Dj Nguli wa Nigeria Jimmy Jatt atakuwepo kuburudisha.
Tuzo hizo zitaruka live kuanzia SAA 12 saa za Afrika Mashariki hadi SAA 4 usiku kupitia Super Sport channel 4 (204),SS 9 (209)ama kupitia Gotv.