Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba weekend hii alimtembelea mama yake Chid Benz na kufanya Mazungumzo ili kuangalia namna ya kumsaidia Rapa huyo pamoja na kuongeza kasi ya kupambana na Magenge ya wauzaji wa Madawa ya Kulevya.
Hatua hiyo imekuja baada ya wiki iliyopita katika mitandao ya kijamii kuzagaa Picha za Rapa Chid Benz "CHUMA" akiwa katika hali mbaya iliyosababishwa na matumizi ya madawa ya kulevya.Baada ya kufanya mazungumzo na mama Chid Benz kupitia mtandao wake wa Instagram Waziri Mwigulu aliandika:
"Nimekutana na kufanya mazungumzo na mama wa msanii Rashid Makwilo Child Benz ambaye kwa sasa amepatwa na tatizo la dawa za kulevya inasikitisha na haivumiliki kuona nguvu kazi ya Taifa inapotea huku wauzaji wakinufaika kwa Pesa haramu.Ifahamike wazi vita ya Serikali dhidi ya Magenge, Wauzaji na wasambazaji wa madawa ya kulevya imeongezeka hasa katika awamu hii ya 5
Chini ya Mh Rais J.P Magufuli.Hivyo anayejihusisha kwa namna yoyote ni vema akaamua kuachana naye kabla hajakutwa na mkono wa dola.Mbali na vyanzo vya taarifa tulivyonavyo ni wajibu
wa kila aliye RAIA MWEMA kutoa taarifa zitakazosaidia kuangamiza biashara haramu ya madawa ya kulevya. Naishukuru familia ya Chid Benz kwa jitihada wanazofanya kuhakikisha kijana mwenzetu anarejea katika hali yake ya kawaida.Unaweza kuimba, unaweza kufanikiwa, unaweza kutatua matatizo yako bila kutumia madawa ya kulevya"alimalizia waziri Mwigulu.
Hali ya Msanii Chid Benz imeendelea kuwa mbaya baada ya kuzagaa taarifa na picha zikimuonesha akiendelea kutumia dawa za kulevya.