MAHREZ ASHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA 2016 HII HAPA ORODHA YA WASHINDI WOTE. | Tino Ze Mastermind

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

MAHREZ ASHINDA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA 2016 HII HAPA ORODHA YA WASHINDI WOTE.

Shirikisho la soka Afrika CAF usiku wa kuamkia Leo limetoa Tuzo kwa wachezaji,timu na waamuzi waliofanya vizuri katika sekta hiyo ya Michezo kwa mwaka 2016.


Hafla hiyo iliyofanyika nchini Nigeria ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Soka lakini pia ikiwa imepambwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali ikiwemo Diamond Platnumz na Rayvanny kutoka Nchini Tanzania.
Wachezaji na timu mbalimbali zilitajwa kuwania tuzo hizo katika vipengele tofauti.Hii hapa chini Orodha ya washindi katika vipengele mbalimbali :

1.Tuzo ya timu bora ya Taifa ya Wanawake ilikwenda kwa Timu ya Nigeria Super Falcons baada ya kutwaa kombe la Afcon kwa mara ya 8.



2.Tuzo ya klabu bora ilikwenda kwa Mamelodi Sundowns Fc ya South Africa baada ya kutwaa kombe la klabu Bingwa Afrika.

3.Kocha bora wa mwaka 2016 ni Pitso Mosimane kutoka Afrika kusini.

4.Tuzo ya Most Promising Talent ilikwenda kwa Kelechi Ihenacho kutoka Nigeria anayeichezea Man City.

5.Mchezaji bora wa kike ni Asisat Oshoala kutoka Nigeria anayekipiga katika klabu ya wanawake ya Arsenal.

6.Mwamuzi bora ni Bakary Papa Gassama kutoka nchini Gambia.

7.Timu bora ya Taifa ya Wanaume ni timu ya Taifa ya Uganda The Cranes.


8.kikosi bora cha mwaka 2016.

9.Mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani ni Denis Onyango kutoka Uganda na klabu ya Mamelodi Sundowns.

10.Mchezaji bora wa Afrika ni Riyad Mahrez kutoka Algeria anayekipiga katika klabu ya Leicester City ya Uingereza.
SHARE HABARI HII NA WENZAKO WAIPATE
KAMA UKIHITAJI KUWEKEWA MUONEKANO MZURI(BLOG DESIGNING) WA BLOG YAKO KAMA HUU WASILIANA NA RUBEN EMMANUEL KWA NAMBA 0716528779/0755542721 KARIBU SANA

google+

linkedin

About Author
  • ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More