Staa aliyewahi kuiwakilisha Tanzania kwenye shindano la Big Brother Africa "The Chase" Nando ameendelea kudhoofika kutokana na matumizi ya Dawa za Kulevya.
Nando aliyewahi kudai kuachana na matumuzi ya dawa za kulevya alikuwa kipenzi cha wasichana wakati anashiriki kwenye shindano hilo alitazamiwa kushinda kabla ya kutimuliwa kutokana na kujihusisha kwenye Ugomvi wa kumtishia kumchoma Kisu mshiriki wa Ghana.Mwishoni mwa wiki zilisambaa Picha Mtandaoni zikimuonesha muonekano wake wa sasa na kuwashtua watu wengi sana.
Kabla ya hapo Nando aliwahi kuhojiwa na kudai kuwa atatoa kitabu chake kiitwacho "Mhuni huyu mwenye akili". Alishwahi kufanya interview "na kuongea sababu za kuingia huku ni Ujana tu mwanangu unajua ujana ni maji ya moto kama watu wanavyosema".
"Na pia ni Pressure na watu niliokuwa nao wakati ule na life niliyoishi mimi ni yale maisha ya kujiachia aliongeza Nando alipoulizwa kilichomfanya ajiingize kwenye matumizi ya Dawa za Kulevya".