Jay Z na mke wake Beyonce wamealikwa katika Sherehe ya kumuaga Rais Barack Obama Ijumaa hii ya Januari 6. kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa na Ikulu ya Marekani Sherehe hiyo itafanyika kwenye viwanja vya Ikulu hiyo ambapo Rais Obama na mkewe Michelle Obama watakuwa washereheshaji.
Mastaa wengine kibao wa Nchi hiyo wamealikwa kuhudhuria kwenye sherehe hiyo akiwemo Stevie Wonder, Usher Raymond, Oprah Winfrey, Samuel L.Jackson,Bradley Cooper na George Lucas.
Obama anatarajia kumkabidhi rasmi madaraka ya kuiongoza Nchi hiyo Rais Mteule Donald Trump Januari 20 baada ya kumaliza miaka minane ya Uongozi wake.