CHADEMA: RAIS MAGUFULI ALIANDIKA RIPOTI YA MCHANGA MWENYEWE. | Tino Ze Mastermind

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

CHADEMA: RAIS MAGUFULI ALIANDIKA RIPOTI YA MCHANGA MWENYEWE.

Katika masuala ya saikolojia (medical psychology) mtu hawezi kupewa mapendekezo zaidi ya 20 halafu akayakubali yote kwa asilimia 100 bila kuwa na chembe ya wasiwasi. Rais aliyakubali mapendekezo yote ya kamati kwa sababu ripoti ile ya uchunguzi wa mchanga wa madini aliiandika yeye mwenyewe, alieleza kiongozi wa CHADEMA.

“Kisaikolojia haiwezekani kitu ambacho hukijui ukakikubali chote bila kuwa na mashaka,” alisema Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Vicent Mashinji.

Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuelezea msimamo wao juu ya sakata la madini ambapo wamesema wao hawawezi kushangilia maneno matupu bali wanasubiria matokeo.
“Tunataka kuona hatua kwanza na sio pongezi ambazo sasa hivi zinaambatana na ushabiki wa kisiasa na kauli tupu nyingi nyingi, mara mwizi, mara mwanaume.”

Aidha, Dkt Mashinji alimtaka Rais Magufuli kuueleza umma wa Watanzania kama kampuni ya Barrick ambao ni wamiliki wakubwa wa Acacia ni wezi au ni wanaume. Akitolea ufafanuzi, neno mwanaume, Dkt Mashinji alisema kwa mazingira ya kitanzania neno mwanaume linamaanisha mtu mchapakazi, mtenda haki, anayejituma. Hivyo Rais aseme kama Barrick ni wezi au wachapakazi.

“Ukiongea katika lugha ya kitanzania ukisema huyu jamaa ni mwanaume kwelikweli, tafsiri yake ni rahisi tu, kwamba huyu jamaa ni mchapakazi, ni muungwana ni mtu wa watu, ndivyo tunavyotumia. Hatuongelei mwanaume kwa sababu ya maumbile yake.“

Wakati huo huo, Dkt Mashinji alisema, kama Rais Dkt Magufuli anawapenda Watanzania kama ambavyo anadai, awape katiba ya Warioba kwani ndiyo chaguo lao na ndio itakayomaliza matatizo yote.
Alisema kuwa, wao waamini kama Rais ataruhusu mchakato wa katiba ya Warioba kupitishwa, basi wabunge wa CCM wanaopitisha sheria kiushabiki na kutotimiza majukumu yao hawatarudi bungeni sababu watawajibishwa na wananchi.

SHARE HABARI HII NA WENZAKO WAIPATE
KAMA UKIHITAJI KUWEKEWA MUONEKANO MZURI(BLOG DESIGNING) WA BLOG YAKO KAMA HUU WASILIANA NA RUBEN EMMANUEL KWA NAMBA 0716528779/0755542721 KARIBU SANA

google+

linkedin

About Author
  • ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More