Msanii wa bongo Flava kutoka Lebo ya WCB Harmonize amesema safari yake ya Miami nchini Marekani ilikuwa ni kwa ajili ya kazi na sio kupumzika huku akitoa sababu za Mpenzi wake Sarah kujumuika naye.
kwamba alienda kutambulishwa nyumbani kwa Mpenzi wake kwani walishafanyaga hivyo siku nyingi.
"Miami nlikuwa nafanya Project sio kupumzika kuna vitu nilikuwa nafanya nina Project kubwa sana mwenyezi Mungu amebariki imeisha salama na nimerudi,nilipokuwa kule Wife alikuwa na Project zake" alisema Harmonize.
"Yeye alikuja kule kwa sababu sasa hivi Italy kuna baridi xana kwa hiyo Miami ni Mji kama una Joto kidogo.Sio utambulisho mbona siku nyingi tushatambulishana,halafu pia alitakiwa asafiri hapa katikati kwa sababu kikishakua kikubwa atazuiwa kupanda Ndege sasa hivi ale good time asafiri asafiri kidogo" alimalizia Harmonize.