GODZILLA AMVAA NIKKI MBISHI KWA MANENO YA VIJEMBE. | Tino Ze Mastermind

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

GODZILLA AMVAA NIKKI MBISHI KWA MANENO YA VIJEMBE.

Rapa Godzilla amemchana kwa mara nyingine mwanafamilia wa Tamaduni Music, Nikki Mbishi akidai kuwa ni mchenguaji asiyekuwa na wimbo mkali (wack rapper).

Zilla amemrushia makombora rapa huyo alipokuwa akifanya mahojiano hivi karibuni na Bongo Dot Home ya 100.5 Times Fm, ambapo alitakiwa kueleza nani mkali wa mitindo huru kati yao. “Nikki Mbishi is just a wack rapper, hana hit song, Nikki mbishi is struggling (Nikki Mbishi anahangaika)".

"Lakini kitu kimoja naweza kumshape nikampatia hit song. halafu sio sehemu nyingine yoyote, nitampigia beat mimi in my own production. I’m gonna make him famous again (nitamfanya kuwa maarufu tena),” alisema Zilla. Aliongeza kuwa wimbo wa mwisho mkali wa Nikki Mbishi alifanya naye, ulikuwa unaitwa ‘Kila Siku’ na baadae akatoa ‘Play Boy’. Lakini sasa anataka kumrudisha kwenye umaarufu.

Wasanii hawa waliwahi kuwa na ushindani mkubwa katika mitindo huru miaka kadhaa iliyopita kabla ya kushirikiana kufanya ngoma kadhaa baadae. Moja kati ya nyimbo zao zilizozua mjadala wa nani amemfunika mwenzie ni ‘Kill Yourself’, ngoma ya Nikki Mbishi aliowapa shavu Mfalme wa Salasala na Cliff Mitindo.

Rapa Godzilla


Nikki Mbishi 
SHARE HABARI HII NA WENZAKO WAIPATE
KAMA UKIHITAJI KUWEKEWA MUONEKANO MZURI(BLOG DESIGNING) WA BLOG YAKO KAMA HUU WASILIANA NA RUBEN EMMANUEL KWA NAMBA 0716528779/0755542721 KARIBU SANA

google+

linkedin

About Author
  • ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More