BIFU LA DIAMOND NA EATV & RADIO LITAWEZA KUMSHUSHA DIAMOND KIMZIKI. | Tino Ze Mastermind

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

BIFU LA DIAMOND NA EATV & RADIO LITAWEZA KUMSHUSHA DIAMOND KIMZIKI.

Bifu la Diamond na Alikiba naliona linafifia kila siku iitwayo leo, huenda likaisha kimya kimya bila hata wao kuonekana wakiwa pamoja katika picha au kufanya wimbo lakini kwa upande wa Diamond namuona kwenye Bifu zito na Ipp Media Especially EATV & RADIO.

IIa bifu la aina hii (Msanii na Media) huwa halizungumziwi sana kwasababu hiyo media yenyewe haitataka msanii huyo asikike kupitia vipindi vyao tofauti na bifu kati ya Msanii na Msanii watawaita kila mmoja kwa wakati wake na kupiga nao story nini chanzo cha bifu lao.

Mara nyingi msanii anapokuwa na bifu na Media hasa ile yenye nguvu na ushawishi, msanii hujikuta akishuka kimuziki. Mfano mzuri #Ruby na #Clouds. Lakini hili la EATV na Diamond kiukweli ni ngumu kutabili itakuwaje kwasababu EATV hawapo vizuri kama zamani na kwa upande wa Diamond yupo vizuri kimuziki na mashabiki zake ambao wapo active sana.

Hivyo ni ngumu kusema kuwa EATV ndio watayumba kwasababu ile ni taasisi na vile vile ni ngumu Diamond kushuka kimuziki kisa EATV kwasababu yupo pamoja na Media yenye nguvu kwasasa (Clouds).

Sijawahi kuona Msanii aliyeshuka kimuziki kisa alikuwa na Bifu na EATV ila CLOUDS….ishawatoa wengi kwenye ramani na Wasanii hao hao EATV walijaribu kuwashika mkono lakini hawakuwa na nguvu hiyo.

SHARE HABARI HII NA WENZAKO WAIPATE
KAMA UKIHITAJI KUWEKEWA MUONEKANO MZURI(BLOG DESIGNING) WA BLOG YAKO KAMA HUU WASILIANA NA RUBEN EMMANUEL KWA NAMBA 0716528779/0755542721 KARIBU SANA

google+

linkedin

About Author
  • ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More