Mwanamuziki Diamond Platnumz ameweka wazi kuwa yeye na aliyekuwa mpenzi wake wa zamani mrembo Wema Sepetu huwasiliana Mara kwa Mara na hukutana kwa siri sehemu ambazo hazina waandishi wa habari au watu wengi.
Akizungumza na kipindi cha XXL cha Clouds Fm Diamond amemwagia sifa mrembo huyo na kusema kuwa amekuwa msaada mkubwa sana kwake hata wakati anaandaa Manukato yake ya "Chibu Perfume".
"Mimi na Wema Sepetu huwa tunawasiliana kwenye simu Mara kwa mara,Mara kadhaa hukutana sehemu ambazo hazina watu wengi kwa sasa tumekua.Kila mmoja wetu anajikita kwenye uhusiano wake Wema Sepetu ana familia yake lakini Uhusiano wetu umejikita katika kusaidiana Kibiashara"alisema Diamond.
Diamond pia aliongeza kwa kusema kuwa Wema Sepetu ndiye aliyemshauri kutumia maneno ya "The Scent You Deserve" kwenye Manukato yake ya Chibu Perfume aliyoyatambulisha hivi karibuni.
Diamond Platnumz na Wema Sepetu walikuwa ni Couple iliyowavutia watu wengi Afrika Mashariki lakini waliachana November 2014 baada ya kuwepo kwa tuhuma za kuchepuka kutoka kila Upande.