Rais wa klabu ya Real Madrid aliyechaguliwa kuendelea kuiongoza klabu hiyo ameweka wazi kwamba mshambuliaji wao raia wa Ureno Cristiano Ronaldo hauzwi.
Hivi karibuni kumekuwepo na taarifa za Ronaldo kutaka kuondoka katika klabu hiyo huku akiusishwa na kutaka kutimkia kwenye klabu yake ya zamani ya Manchester United. Sababu za Ronaldo kutaka kuondoka kwenye klabu hiyo ni kutokana na kukasirishwa na kitendo cha mamlaka nchini Hispania kumtuhumu kukwepa kodi na klabu yake kutompa ushirikiano kwenye sakata hilo.
Florentino Perez amesistiza kuwa mambo yote yatakuwa sawa baina ya Ronaldo na Real Madrid na mchezaji huyo atabaki kwenye klabu hiyo.