Baada kuipa mafanikio makubwa klabu yake ya Real Madrid ya Spain, Cristiano Ronaldo ameutaarifu uongozi wa klabu hiyo kuwa anataka kuondoka. Gazeti la A Bola la Ureno limeripoti na kuzihusisha klabu za PSG na Manchester United kuwa ni timu ambazo huenda akajiunga nazo.
Hatua hii ya Ronaldo ambaye pia ni mshindi mara nne wa tuzo ya 'Ballon d'or' inakuja baada ya kupata kesi ya ukwepaji kodi. Katika hatua nyingine gazeti la Marca limeripoti tetesi kuwa Real Madrid imeiambia Man United iandae Pauni 160 milioni, kama inamtaka mkali huyo.
Cristiano Ronaldo licha ya kutetewa na club yake ya Real Madrid kuhusiana na tuhuma za ukwepaji kodi zinazomkabili, ameripotiwa kufikiria kufanya maamuzi magumu.
Cristiano Ronaldo ambaye ni mchezaji tegemeo katika kikosi cha Real Madrid anatuhumiwa kukwepa kodi nchini
Hispania katika kipindi kati ya 2011 hadi 2014 kiasi kinachotajwa kufikia pound milioni 13 ambazo ni zaidi ya Bilioni 35 za kitanzania.
Mtandao wa Sky Sports umeripoti kuwa staa huyo aliyeisaidia Real Madrid kutwaa mataji matatu ya UEFA Champions League anataka kuondoka yeye mwenyewe
Hispania kutokana na tuhuma zinazoendelea ambazo anaamini hafanyiwi haki.