Mtu mmoja mwenye asili ya Tanzania, Omega Mwaikambo (43) amehukumiwa kufungwa jela miezi mitatu baada ya kupatikana na hatia ya kuposti kwenye mtandao wa Facebook picha za mwili wa mtu aliyefariki katika ajali ya moto katika jengo la Grenfell Tower iliyotokea katika jiji la London nchini Uingereza.
Omega alipatikana na kosa hilo la kimtandao baada ya yeye mwenyewe kukiri kosa hilo kwa utetezi wa kuwa alifanya hivyo ili kurahisisha utambuzi wa mwili wa marehemu huyo.
Hata hivyo utetezi huo haukutosha kuifanya Mahakama kutomtia hatiani.