Tino Ze Mastermind: June 2017

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

HAWA NDIYO MAPACHA WA CHRISTIAN RONALDO.

Mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo ameamua kuwaweka wazi watoto wake mapacha ambao amewapata hivi karibuni.

Ronaldo ameamua kuwaweka wazi mapacha wake hao mitandaoni baada ya hapo jana kuthibitisha kupata watoto hao wakati timu yake ya taifa ya Ureno ilipotolewa kwenye michuano ya kombe la mabara katika ngazi ya timu za taifa.

“So happy to be able to hold the two new loves of my life ,” ameandika mchezaji huyo kwenye picha  aliyoiweka kwenye mtandao wa Instagram.

Watoto hao wanaungana na kaka yao Cristiano Jr mwenye miaka saba. Wakati huo huo mpenzi wa Ronaldo, Georgina Rodriguez ambaye ni mwanamitindo anadaiwa kuwa na ujauzito wa miezi mitano.

BIFU LA DIAMOND NA EATV & RADIO LITAWEZA KUMSHUSHA DIAMOND KIMZIKI.

Bifu la Diamond na Alikiba naliona linafifia kila siku iitwayo leo, huenda likaisha kimya kimya bila hata wao kuonekana wakiwa pamoja katika picha au kufanya wimbo lakini kwa upande wa Diamond namuona kwenye Bifu zito na Ipp Media Especially EATV & RADIO.

IIa bifu la aina hii (Msanii na Media) huwa halizungumziwi sana kwasababu hiyo media yenyewe haitataka msanii huyo asikike kupitia vipindi vyao tofauti na bifu kati ya Msanii na Msanii watawaita kila mmoja kwa wakati wake na kupiga nao story nini chanzo cha bifu lao.

Mara nyingi msanii anapokuwa na bifu na Media hasa ile yenye nguvu na ushawishi, msanii hujikuta akishuka kimuziki. Mfano mzuri #Ruby na #Clouds. Lakini hili la EATV na Diamond kiukweli ni ngumu kutabili itakuwaje kwasababu EATV hawapo vizuri kama zamani na kwa upande wa Diamond yupo vizuri kimuziki na mashabiki zake ambao wapo active sana.

Hivyo ni ngumu kusema kuwa EATV ndio watayumba kwasababu ile ni taasisi na vile vile ni ngumu Diamond kushuka kimuziki kisa EATV kwasababu yupo pamoja na Media yenye nguvu kwasasa (Clouds).

Sijawahi kuona Msanii aliyeshuka kimuziki kisa alikuwa na Bifu na EATV ila CLOUDS….ishawatoa wengi kwenye ramani na Wasanii hao hao EATV walijaribu kuwashika mkono lakini hawakuwa na nguvu hiyo.

NDUGU WASIMULIA JINSI VIONGOZI WAWILI WALIVYOUAWA "KIBITI" HUKU MMOJA AKITOBOLEWA MACHO YOTE.

Ndugu Wasimulia Jinsi Viongozi Wawili Walivyouawa KIBITI Huku Mmoja Akitobolewa Macho Yote

Risasi tano zimetumika kuwaua Mwenyekiti wa Kijiji cha Mangwi na Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, kisha kumjeruhi machoni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Londo, wilayani Kibiti, mkoani Pwani.

Waliofariki katika tukio hilo ni Ofisa Mtendaji, Mwarami Shamte aliyekutwa na majereha matatu ya risasi na Mwenyekiti wa Kijiji, Hamis Bakari Mkima aliyekutwa na jeraha moja.

Pia wauaji hao walimpiga, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Londo, Michael Martin risasi ya macho, iliyoharibu macho yake mawili.

Kama hiyo haikutosha, waliichoma moto nyumba ya Martin na kisha kutokomea kusikojulikana.

Mganga wa zamu katika Kituo cha Afya Kibiti, Dk Sadock Bandiko alithibitisha kuuwawa kwa viongozi hao wa kijiji hicho.

Amesema Shamte amekutwa na majeraha matatu yaliyotokana na kupigwa risasi.

“Shamte alipigwa risasi moja kichwani na risasi mbili tumboni,”amesema.

Kwa upande wa mwenyekiti wa kijiji hicho, Dk Sadock amesema marehemu alipigwa risasi moja ya shingoni aliyopigwa toka upande wa kulia na kwenda kushoto lakini  haikutokeza.

Pia alisema mwenyekiti huyo alikuwa na jeraha kubwa katika mguu wake wa kushoto lililotokana na kukatwa na kitu chenye ncha kali.

Mganga Mkuu wa Hospital ya Mchukwi, Dk Zacharia Lukeba alipolazwa Martin, amesema alipigwa risasi moja ya kichwani iliyofumua na kuharibu kabisa macho yake.

Amesema tayari wamempa rufaa kwenda Hospital ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Mmoja wa ndugu za marehemu hao amesema watu wanne waliokuwa na bunduki wakiwa wamevaa nguo nyekundu na kuficha sura zao kwa soksi walivamia kijijini hapo saa nne usiku wa kuamkia jana.

Amesema watu hao walianza kwenda kwa Mwenyekiti wa Kijiji hicho (Hamis Bakari Mkima) (30) ambaye alifanikiwa kuwakimbia kabla hawajamfikia.

Amesema watu hao walimpiga na kitu chenye ncha kali katika mguu wake wa kushoto kisha kumrejesha kwake huku wakimtaka awapeleke kwa viongozi mbalimbali wa kijiji hicho.

Alieleza kuwa baada ya hapo walimtaka awapeleke kwa Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho (Mwarami Shamte) (40) na baada ya kufika huko walimpiga risasi tatu na alifariki dunia papo hapo.

Amesema watu hao bado walimtaka mwenyekiti huyo awapeleke kwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Londo na baada ya kufika kwake walimpiga risasi ya usoni iliyoharibu macho yake.

Amesema baada ya hapo walimpiga risasi moja mwenyekiti huyo wa Kijiji cha Mangwi, (Hamis Mkima) na alifariki papo hapo.

Pia ameeleza kuwa wakati watu hao wakifanya hayo walikuwa tayari wamechoma moto nyumba ya Mwenyekiti wa Kitongoji cha Londo kwa kutumia mafuta ya petroli yaliyokuwemo kwenye pikipiki yake na kuteketeza kabisa nyumba yake yote.

Mdogo wa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Londo (aliyepofuliwa macho) aliyejitambulisha kwa jina la Paul Martin amesema tukio hilo limetokea usiku wa jana saa 4  ikiwa ni muda mfupi tangu aagane na kaka yake.

“Nilikuwa nyumbani kwake na nimeondoka wakati huo huo  kwenda kulala baada ya dakika chache kupita, tulianza kusikia kelele za watu nisiowafahamu wakiwa kwenye nyumba ya kaka yangu,” amesema.

Paul amesema baada ya kusikia kelele hizo alitoka nje ili ashuhudie lakini kabla hajafanya lolote aliwekwa chini ya ulinzi kwa kumulikwa tochi na kutishiwa kupigwa risasi.

"Niliona watu kama watano wakiwa na silaha ambao waliniweka chini ya ulinzi baada ya kunimulika tochi," alisema.

Amesema baadhi ya watu hao walikuwa ndani ya nyumba ya kaka yake wakiendelea kumhoji huku wakiwa wamefunika sura zao.

Ameongeza kuwa baada ya hapo watu hao waliondoka na kaka yake kwenda kusikojulikana na baada ya muda mfupi walirudi naye.

Amesema watu hao baada ya kurejea naye waliwaamrisha watoto wake waliokuwa wamelala kutolewa nje kisha walichukua mafuta ya petroli yaliyokuwa kwenye pikipiki ya kaka yake kisha kuyamwaga ovyo kwenye nyumba hiyo na kuichoma moto.

Amesema baada ya tukio hilo waliondoka naye kwa mara ya pili na kwenda naye kusikojulikana kisha wakampiga risasi ambayo imeharibu macho yake yote.

Amesema baada ya kumpiga risasi hiyo walimtelekeza katika barabara iendayo katika kijiji cha Misimbo ambapo walimkuta jana  asubuhi akiwa hajitambui.

Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Onesmo Lyanga alithibitisha kutokea kwa matukio hayo.

USAJILI : TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA MPAKA SASA.

Mchakato wa Manchester United kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, mwenye umri wa miaka 24, unasuasua baada ya Real kupandisha dau la mchezaji huyo hadi karibu pauni milioni 80 (Mirror).

Mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata Morata ambaye ameoa hivi karibuni, amelazimika kuondoka kwenye fungate yake ili kuharakisha uhamisho wake kwenda Old Trafford (AS). Wasiwasi kuhusu hatma ya Cristiano Ronaldo unasababisha kuchelewa kutangazwa kwa uhamisho wa Alvaro Morata kutoka Real Madrid kwenda Manchester United.

Tottenham wapo tayari kumpa mkataba mpya beki wake Toby Alderweireld, 28, ambaye ananyatiwa na Inter Milan (Daily Mirror).

Mshambuliaji wa Sunderland Jermain Defoe, 34, amekwama kwa sababu Bournemouth na West Ham zinachelea kumchukua kutokana na gharama kubwa za mchezaji huyo (Daily Star). Mshambuliaji wa Burnley Andre Gray, 26, anataka mkataba mpya wenye mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki, lakini klabu hiyo inasema haina uwezo wa kumlipa (Daily Star).

Fernabahce ya Uturuki inafikiria kupanda dau la kumchukua winga wa Everton Kevin Mirallas, 29 (Fanatik). AC Milan wamejitoa katika mbio za kutaka kumsajili kiungo wa Real Madrid, James Rodriguez, 25, na hivyo kuwapa matumaini zaidi Chelsea na Manchester United (Mundo Deportivo).

Everton wamewazidi kete Manchester United katika kumsajili beki Michael Keane, 24, kutoka Burnley na anatarajiwa kutua Goodison Park siku chache zijazo (Sun). AC Milan wanataka kumsajili beki wa kati wa Arsenal, Laurent Koschielny, 31 (Telefoot).

Mchezaji wa klabu ya Arsenal Laurent Koschielny (wapili kulia) Aston Villa watakamilisha usajili wa beki John Terry, 34, wiki hii ambapo mkataba wake na Chelsea unamalizika (Daily Mirror). Manchester United bado wataendelea kujaribu kumsajili kiungo wa Monaco Fanbinho, 23, licha ya kumchukua Nemanja Matic, 28, kutoka Chelsea.

Jose Mourinho huenda akamchezesha Fabinho kama beki wa kulia (Independent). Mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial umri miaka 21, atamwambia Jose Mourinho kuwa anataka kuondoka, na klabu hiyo haitamzuia kuondoka OT (Daily Express). Manchester United wamepanda dau la euro milioni 80 kumtaka kiungo wa Real Madrid James Rodriguez (Mediaset Premium).

Francesco Totti, 40, anazungumza na klabu ya Tokyo Verdy kuhusu mkataba wa pauni 50,000 kwa wiki. Totti anaondoka Roma baada ya miaka 25 (Sun). Barcelona wamejiwekea makataa ya siku 10 wawe wamemsajili beki wa Arsenal Hector Bellerin na siku hizo zikipita bila kumpata wataelekeza macho yao kwingineko (Mundo Deportivo). Arsenal wana uhakika Alex Oxlade-Chamberlain atasaini mkataba mpya wa pauni 100,000 kwa wiki, lakini mchezaji huyo anataka kwanza kuhakikishiwa nafasi kabla ya kusaini (Evening Standard).

Zinedine Zidane hana mpango wa kumuuza Gareth Bale msimu huu, licha ya taarifa kuwa Real wanataka kumsajili Kylian Mbappe (Marca). Beki wa Chelsea Kurt Zouma, 22 huenda akajiunga na Nice kwa mkopo akisaka kucheza katika kikosi cha kwanza (TalkSport).

Kurt Zouma au Michy Batshuayi, mmoja wao huenda akauzwa Sevilla, kama sehemu ya mkataba wa Chelsea kumsajili winga Vitolo (Express). Manchester United wanataka kumsajili kiungo wa Middlesbrough Marten de Roon, 26, na wanaamini anaweza kupatikana kwa pauni milioni 8.8 (Tutto Mercato).

Chelsea, Tottenham, Everton, Leicester, Southampton na Stoke, zote zinamtaka Ben Gibson, 24, lakini watalazimika kulipa pauni milioni 25 kumpata beki huyo wa Middlesbrough (Daily Star). Tottenham wanamtaka beki wa Southampton Cedric Soares, 25, lakini wanakabiliwa na upinzani kutoka Barcelona na Juventus (Daily Mirror Kiungo wa Leicester Nampalys Mendy, 25, anataka kwenda Bordeaux baada ya kushindwa kucheza vizuri England (L’Equipe).

Barcelona wamekasirishwa na nahodha wao wa zamani Carlos Puyol, baada ya mmoja wa mabeki anaowawakilisha mwenye umri wa miaka 16, Eric Garcia kuamua kuitosa Barcelona na kwenda Manchester City (Independent). Paris Saint-Germain wanajiandaa kutoa euro milioni 240 kujaribu kuwashawishi Kylian Mbappe na kipa Gianluigi Donnarumma.

PSG watatoa euro milioni 135 kwa ajli ya Mbappe na euro milioni 39 kwa ajili ya kipa wa AC Milan Donnarumma, na pia wanataka kutoa euro milioni 42 kumtaka Fabinho wa Monaco na euro milioni 23 kumchukua Raphael Guerrerro kutoka Borussia Dortmund (Sport).

Tianjin Quanjian ya China iko tayari kurejea tena katika mbio za kutaka kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre Emerick-Aubameyang na wapo tayari kutoa euro milioni 80 (SportBild).



MANENO YA DIAMOND MARA BAADA YA RAYVANNY KUCHUKUA TUZO YA BET.

Msanii wa Bongo Flava, Rayvanny kutoka Wasafi Classic Baby (WCB) ameshinda tuzo ya BET (Black Entertainment Television) kipengele cha ‘Viewers Choice Best New International Act Artist’.

Kufuatia ushindi huo msanii Diamond Platnumz ambaye anaiongoza WCB amepongeza ushindi huo wa Rayvanny, amesema kuwa zaidi ya miaka mitatu tunaenda na kurudi patupu lakini safari hii si patupu tena kufuatia ushindi huo.

“Hatimaye leo Unakuja nayo Tanzania Dah! ….Zaidi ya miaka mi 3 tunaenda na kurudi Patupu….Hakika Maisha Uvumilivu na kutokata tamaa…. BRING IT HOME BOSS!!! @babutale” “WOOOOOOOOOYOOOOOOOO!!!!!!!….. Nikishindwa kwa Mkono wa Kulia, ntatumia hata Mkono wa Kushoto…..ila lazma ifike @Wcb_Wasafi TANZANIA!!!! Chkua hiyo #Wcb_Wasafi #WinningTeam!”



TID AFUNGUKA MARA BAADA YA QUICK RACKA NA OMG KUTUMIA KUTUMIA CHORUS YAKE BILA RUHUSA.

Leo June 24, 2017 upepo wa Bongofleva huenda ukaenda sivyo kwenye studio za Switch Records ikiwa ni mastaa tu tangu Quick Rocka na kundi la OMG waachie video yao mpya “Watasema”

Ambayo wametumia melody na maneno ya wimbo wa zamani uliofanywa na TID “Watasema Sana” na inaonekana TID hajashirikishwa na kuamua kudai haki zake. TID ameandika

“Wat is this….?! Hivi ndio mnapata Magari yenu!? @quickrocka & @omgtanzania we need to TALK #Watasema Naomba tukutane Central Police huwezi kutumia Haki zangu hivihivi Kabla sijafanya kitu kibaya nahitaji million 20 compensation… This song ni Awards mbili Za Kisima Music Awards 2005 in Kenya u can’t just Steal it, Unalala Ndani Leo – alimalizia  TID.

TETESI TETESI ZA USAJILI MPAKA SASA BARANI ULAYA.

Katika dirisha hili la usajili, klabu ya Portsmouth imetangaza kumsajili beki Nathan Thompson kwa mkataba wa miaka miwli.

Na kiungo wa klabu ya Gillingham, Elliot List amekubali kuongeza mkataba wa mwaka mmoja ndani ya klabu hiyo, kwa mkataba huo utamfanya adumu mpaka mwisho wa msimu wa mwaka 2017/18.

Mchezaji wa klabu ya Chelsea, Diego Costa Diego Costa amesema anahitaji kusaini kwa miamba ya Hispania timu ya Atletico Madri, mchezaji huyo aliondoka Atletico mwaka 2014.

Hawa ni wachezaji 10 waliogonga vichwa vya habari katika dirisha la usajili barani Ulaya siku ya leo

New Audio _ Chid Benz feat Q_ Chilah _ MUDA

Download Diamond Platnumz Feat Tiwa Savage _ Fire


          DOWNLOAD AUDIO

Download New audio _ Diamond Platnumz I miss You

 
        DOWNLOAD AUDIO

EXCLUSIVE : DIAMOND PLATNUMZ AMKANA HAMISA MOBETTO.

Msanii wa muziki Diamond Platnumz amekanusha taarifa ambazo zimekuwa zikizagaa katika mitandao ya kijamii kuwa Hamisa Mobeto ana mimba yake. Aidha muimbaji huyo amekanusha pia kuwahi kutoka kimapenzi na video queen huyo ambaye anatikisa katika tasnia ya urembo.

Akiongea katika kipindi cha XXL cha Clouds Fm Jumatano hii wakati akiutambulisha wimbo wake mpya ‘I Miss You’, Diamond amedai tetesi za yeye kutoka kimapenzi na Hamisa zilianza baada ya kufanya naye kazi katika project ya wimbo, Salome.

“Toka nimeshoot na Hamisa Mobeto wimbo wa Salome, watu wamekua wakituhusisha pamoja, ujauzito wa Hamisa sio wangu,” alisema Diamond. “Jamani mwenye mimba si ajitokeze, si unajua hata mtu wake atakuwa anajisikia vibaya,” Pia muimbaji huyo amedai wasichana wengi ambao anafanya nao kazi upakaziwa kuwa anatoka nao kimapenzi.

"Picha za Zari akiwa kwenye bwawa la kuogelea niliziona mtandaoni, nikapanic sana nikadhani kwamba Mama watoto wangu kazingua, lakini baadae nilifahamu kwamba hakukuwa na tatizo katika picha, kwani yule jamaa ni shemeji yake na hawakufanya lolote baya




Diamond Platnumz akiwa studio Leo.

MTOTO ALIYEKUWA ANAKUNYWA MAFUTA SUKARI NA MAZIWA ARUHUSIWA MHN.

Mtoto aliyekuwa akinywa mafuta na sukari, Shukuru Kisonga (16) ameruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) baada ya kupatiwa matibabu na afya yake kuimarika. 

Aidha Shukuru alifikishwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mei 16, mwaka huu akitokea Tunduru ambako aliripotiwa kuishi kwa kunywa mafuta, sukari na maziwa. Baada ya kufikishwa MNH alifanyiwa uchunguzi na timu ya madaktari Bingwa na kubaini kwamba ana ugonjwa wa Selimundu pamoja na upungufu wa madini ya chuma na kwamba upungufu wa madini hayo ulisababisha anywe mafuta, sukari na maziwa.

“Kwakweli namshukuru Mungu, pia nawashukuru sana madaktari na wauguzi wa Muhimbili kwani hali ya mwanangu ilikuwa mbaya, alikuwa hawezi kula chochote zaidi ya kunywa mafuta, maziwa na sukari, lakini baada ya kupatiwa matibabu, afya yake imeimarika na sasa anaweza kula vyakula vyote,’’ amesema Mama Shukuru.

Hata hivyo, Awali mtoto Shukuru alipelekwa katika Hospitali ya Misheni Tunduru kwa ajili ya kupatiwa matibabu, lakini ugonjwa haukooneka na baadaye alipelekwa hospitali Nyangao mkoani Lindi.

Mtoto Shukuru akiwa na mama yake.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO JUNE 21, 2017.

Nimekusogeze kurasa za Magazeti ya Leo Jumatano June 21 kuanzia Vichwa vya Habari vya Siasa Jamii na Michezo.

DIAMOND PLATNUMZ KULIACHIA DUDE KESHO.

Ni kweli Diamond Platnumz  anataka kuachia ngoma mpya Jumatano hii? Kama haufahamu hilo basi kaa tayari kulipokea hilo.

Msanii huyo amekuwa akiteka vichwa vya habari kila anapokaribia kuachia ngoma zake mpya kutokana na style anazotumia. Kupitia mtandao wa Instagram, Diamond ameahidi kuachia wimbo wake huo siku ya kesho.

“@sallam_sk punguza Hasira  Xxl ya @Cloudfmtz na @Bdozen saba hadi Kumi Kamili Kesho….. ameandika Diamond katika mtandao huo.



PICHA : SHABIKI MAARUFU WA YANGA ALLY YANGA AFARIKI DUNIA KWENYE AJALI YA GARI DODOMA.

Shabiki wa Yanga maarufu kwa jina la Ally Yanga amefariki dunia leo katika ajali ya gari. Ally Yanga alijizolea umaarufu mkubwa katika tasnia ya soka kotokana na jinsi alivyokuwa akivaa na kujichora pamoja na namna yake ya ushangiliaji anapokuwa uwanjani.

Ajali hiyo iliyohusika katika kifo cha Ally Yanga imetokea leo mkoani dodoma.

Klabu ya Yanga kupitia Idara ya Habari na mawasiliano wametuma salamu za rambirambi kwa ndugu na jamaa wa Ally Yanga kufuatia kifo cha mpendwa wao ambapo wamesema kuwa faraja ya Mungu ikawe na familia hiyo katika kipindi hiki kigumu.

“Uongozi wa Yanga SC umepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Ally Yanga, hakika Mungu ni mwema, faraja ya Mungu wetu ikawe kwa familia katika kipindi chote cha majonzi kwa kuondokewa na mpendwa wao.”

Aidha, kwa upande wao, Yanga wamesema kuwa wameachwa na pengo kubwa kutokana kutokana na kupoteza shabiki na mwanachama huyo maarufu.

“Pia nasi Yanga kifo chake kina acha pengo kubwa kwa nafasi yake ambayo ilipelekea kujipatia umaarufu mkubwa na alikuwa balozi mzuri kama mwanachama na shabiki mkubwa wa timu yetu, Bwana alitoa, Bwana ametwaa.”

Ally Yanga Enzi za Uhai wake


PEREZ : RONALDO HAUZWI.

Rais wa klabu ya Real Madrid aliyechaguliwa kuendelea kuiongoza klabu hiyo ameweka wazi kwamba mshambuliaji wao raia wa Ureno Cristiano Ronaldo hauzwi.

Hivi karibuni kumekuwepo na taarifa za Ronaldo kutaka kuondoka katika klabu hiyo huku akiusishwa na kutaka kutimkia kwenye klabu yake ya zamani ya Manchester United. Sababu za Ronaldo kutaka kuondoka kwenye klabu hiyo ni kutokana na kukasirishwa na kitendo cha mamlaka nchini Hispania kumtuhumu kukwepa kodi na klabu yake kutompa ushirikiano kwenye sakata hilo.

Florentino Perez amesistiza kuwa mambo yote yatakuwa sawa baina ya Ronaldo na Real Madrid na mchezaji huyo atabaki kwenye klabu hiyo.

Christian Ronaldo akiwa na Florentino Perez

MAGAZETI YA LEO JUMANNE JUNE 20, 2017.

Nimekusogezea Kurasa za Magazeti Ya Leo Tanzania June 20 Jumanne kuanzia vichwa vya Habari vya Siasa Jamii na Michezo.