Tino Ze Mastermind: November 2016

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Kiasi cha fedha alichochangia Ronaldo kwa klabu ya Brazil iliyopata Ajali ya Ndege.

Nahodha wa wa timu ya taifa ya Ureno na mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Christian Ronaldo ameeleza majonzi yake kufuatia msiba uliokumba ulimwengu wa soka baada ya Wachezaji na Viongozi wa klabu ya Chapecoense ya Nchini Brazil kufariki kutokana na Ajali ya Ndege.

Ronaldo ameamua kuchangia kiasi cha euro milioni 3 kwa timu hiyo kama Mchango wake wa rambirambi ambazo ni zaidi ya bilioni 9 za kitanzania kwa ajili ya kusaidia klabu hiyo na wale wote waliofikwa na msiba huo.Kwa upande mwingine klabu nyingine za Brazil zimeliomba shirikisho la soka nchini hump kuziruhusu kuichangia klabu hiyo ya Chapecoense wachezaji bure na pia
Isisushwe daraja katika kipindi cha miaka 3.Aidha waliokuwa wapinzani wao
Katika Final hiyo wameliomba shirikisho la soka barani humo,kuipa klabu ya Chapecoense kombe hilo.Kati ya wachezaji waliokuwa na klabu hiyo ni 3 tu wamesalia ambao kutokana na sababu mbalimbali hawakuwepo safarini kwenda Colombia.Mamia ya Mashabiki wamekusanyika katika Uwanja wa timu hiyo nchini Brazil kuwaombea wale wote waliofariki.Nimekusogezea picha hapa chini kuona kinachoendelea nchini Brazil:

Ali kiba asherekea siku yake ya kuzaliwa Mbugani,Jokate atuma ujumbe mzito kwake.

Mkali wa Bongo flava Ali kiba jumanne hii aliungana na uongozi wake na familia yake kwenda mbuga za wanyama za Serengeti National Park mkoani Mara kwa ajili ya kusherekea siku yake muhimu katika maisha yhuku 

Mkali huyo wa Aje ametimiza miaka 30
amesema ameamua kufanya birthday yake mbugani kama moja ya kutumia jina lake kutangaza Utalii wa ndani"Namshukuru sana Mungu kwa kunifikisha miaka hii,familia yangu na mama yangu,nimeamua kusherekea birthday yangu mbugani ili kutangaza Utalii wa ndani kupitia jina langu"alisema
Ali kiba.Wakati huo huo mwanadada jokate au JoJo ametumia lugha ya  kifaransa kuwasilisha Ujumbe wake huku akijaribu kutomwaga mchele kwenye kuku wengi jojo ameandika
Lakini shabiki mmoja anayeielewa lugha hiyo ametafsiri post yake kwa kingereza
inayosema "baby happy birthday I love you so much it is paining,I hope that French has sang,you prepare for that but
I want nothing but the best for you from the bottom of my heart the rest I leave to God for what happens to know that jojo doesn't disturb and that am happy to have you as my friend rest blessed"mwisho wa kunukuu.
Alikiba amefanya sherehe hiyo katika eneo la mpakani mwa Tanzania na Kenya katika eneo la Masai Mara kwenye Camp ya Sayari.Nimekusogezea picha ya yaliyotokea kwenye sherehe hiyo.

Picha ya Diamond akiwa amevaa Kiboxer yasababisha povu zito Instagram.

Mwanamuziki Diamond Platnumz amejikuta akitupiwa lawama baada ya kupiga picha akiwa amevaa kiboxer.Diamond ambaye ni bingwa wa kusababisha povu kwenye mitandao ya kijamii.Kwenye picha hiyo aliyoweka Instagram Diamond aliandika "Straight from changing room.....I think I need to go back to the gym so that i can be more flexible on m 24th Pre_Xmass Performance in Dar es salaam" alimalizia Diamond.

Licha ya kufunika na Emoji kwenye eneo la sehemu za siri,selfie hiyo imesababisha hisia tofauti huku wengine
wakimponda staa huyo kwa kukosa staha.Hizi ni baadhi ya comments na mapovu ya watu Instagram.





POLISI YAZUNGUMZIA SAKATA LA ASKARI ALIYEJIUA KWA BAHATI MBAYA.

Jeshi la polisi mkoani Pwani limezungumzia kifo cha askari wake PC Armand Furaha 33 aliyejipiga risasi kifuani bila kukusudia na kufariki dunia.Askari huyo alijipiga risasi hiyo usiku akiwa anaelekea kwenye lindo nyumbani kwa mkuu wa Wilaya ya Kibaha.Tukio hilo lilitokea saa 1 usiku eneo la Maili moja wakati askari huyo akiwa njiani
kuelekea kwenye kituo cha lindo alichopangiwa.

Kaimu kamanda wa polisi Pwani Blasius Chatanda amesema askari huyo alijipiga risasi kwa bahati mbaya kwa bunduki aina ya SMG akiwa amekaa kwenye kiti cha mbele katika gari alilokuwa anasafiria kwenda lindoni.Amesema uchunguzi wa awali umebaini "kuwa askari huyo alikuwa tayari ameweka risasi chemba kwenye bunduki hiyo aliyokuwa nayo na kwa bahati mbaya akiwa anashuka kwenye hilo gari ndipo risasi hiyo ikafyatuka na kumpiga kifuani eneo la kushoto na kufa wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Tumbi".

Kabla ya tukio hilo askari huyo aliwasili kazini jioni na kukuta amepangiwa kituo cha ulinzi cha Mkuu wa Wilaya hivyo kama ilivyo ada alichukua zana za kazi ikiwemo bunduki hiyo na kuanza safari ya kuelekea lindoni kwake huko kwa DC.
Lakini kwa bahati mbaya hakufika alikufa kwa kujipiga risasi bahati mbaya amesema Chatanda.
Akizungumzia suala la kujipiga risasi msemaji wa jeshi la Polisi,Advera Bulimba amesema kila tukio hutokana na mazingira tofauti.

Magazeti ya leo Nov 30 Jumatano #Headlines

Nimekusogezea kurasa za mbele za Magazeti ya leo Nov 30 Jumatano kama yalivyochapishwa yakihusisha Siasa Jamii na Michezo.

Wananchi wa Cuba watoa Heshima zao za Mwisho.

Maelfu ya raia wa Cuba wametoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi mwanamapinduzi Fidel Castro aliyeaga dunia siku ya ijumaa akiwa na umri wa miaka 90.Raia wengi wa Cuba walikuwa katika milolongo mirefu ya foleni kabla hata ya Alfajiri ili kuhakikisha wako miongoni mwa watu wa kwanza kutoa heshima zao.Katika uwanja wa Revolution Square katika mji Mkuu Havana sehemu ambayo waombolezaji wameweka picha ya kiongozi huyo akiwa ameshika bunduki.

Ilikuwa siku ya kwanza ya kipindi cha siku 6 za maombolezi rasmi ya kifo cha
Fidel Castro.Siku za maombolezi zitakamilika baada ya majivu ya mwili wake kuzikwa siku ya Jumapili.Majivu ya Fidel Castro yatatazamiwa kuwasilishwa kwa umma katika Uwanja wa Revolution Square lakini yatawekwa katika sehemu tofauti.

Ndege iliyobeba Wachezaji wa timu ya soka ya Brazil yaanguka Colombia

Ndege iliyokuwa imewabeba watu 81 wakiwemo wachezaji na maafisa wa moja ya klabu kubwa za soka nchini Brazil imeanguka ikikaribia mji wa Medelin nchini Colombia na kuua watu 76.Polisi wamesema watu 5 walinusurika lakini wengine wote waliangamia.Ndege hiyo ya kukodishwa ilikuwa safarini kutoka Brazil ikipitia Bolivia na ilikuwa imewabeba wachezaji na Maafisa wa timu ya Chapecoense.

Klabu hiyo ilikuwa imepangiwa kucheza mechi ya final ya Copa Sudamericana dhidi ya timu ya Atletico Nacional ya mji wa Medellin.Mechi ya awamu ya kwanza ya kombe hilo,la pili kwa umuhimu America Kusini ilikuwa imepangwa kuchezwa jumatano lakini sasa imesitishwa.Timu hiyo inayotoka mji wa 
Chapeco kusini mwa Brazil ilipandishwa kucheza ligi ya daraja la kwanza nchini Brazil mwaka 2014 na ilifika fainal ya kombe hill la Sudamericana kwa kuilaza San Lorenzo ya Argentina.Maafisa wa klabu hiyo ya Chapecoense wametoa taarifa wakisema "tunamuomba mungu awe na wachezaji maafisa,wanahabari na wageni wengine na watu ambao waliandamana na timu yetu.

Kurasa za Magazeti ya leo Nov 29 Jumanne #Headlines

Nimekukusanyia vichwa vya habari vya Magazeti ya Leo Nov 29 Jumanne kuanzia Siasa Jamii na Michezo.

Matokeo ya Mechi zote za Jumamosi na Jumapili na Msimamo.

Nimekukusanyia Matokeo ya Mechi zote za ligi mbalimbali barani Ulaya zilizofanyika Jumamosi na Jumapili na msimamo wa nani kinara na wa mwisho kwenye ligi kama ifuatavyo:
  England : Premier League

Matokeo

Msimamo
Spain : Premier Division
Msimamo

Germany : Bundesliga
Msimamo

France : Ligue 1
Msimamo