RUGE AZUNGUMZIA UGOMVI WAKE NA LADY JAYDEE NA RUBY | Tino Ze Mastermind

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

RUGE AZUNGUMZIA UGOMVI WAKE NA LADY JAYDEE NA RUBY

Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds media Group CMG bwana Ruge Mutahaba amefunguka kwenye interview aliyowafanya kwenye kituo cha radio Clouds na kufunguka mambo mbalimbali yanayozungumzwa juu yake.

Alipoulizwa juu ya suala la ugomvi wake na lady jaydee na kwanini radio yao ya Clouds haichezi ngoma za lady jaydee alijibu "tatizo ni kwamba hakuna ambacho hatujamaliza tulimaliza tunasubiri Order unajua kimsingi ulipopewa Order ya kwamba nyimbo zangu usipige jina langu usiseme kwenye chombo chako vyovyote itakavyokuwa mimi sitaki kusikia hiyo kitu hiyo ndio Order.Kwa hiyo tukikutana
nimuombe tena Lady Jaydee kama
tutaruhusiwa kufanya hiyo kitu.Ruge pia
amesema ana mda mrefu hujawahi kukutana na Lady jaydee "Sina tatizo na lady jaydee kesi yetu ilikuwa mahakamani na hukumu imeshatolewa
na yeye alikiri kuwa maneno aliyosema
alisikia kwa watu tu".Pia Ruge alisema "hata leo ukinipa nafasi ya kunywa naye
Kahawa npo tayari nitashukuru sana  kwa huo mwaliko".

Alipoulizwa kuhusu suala la Ruby kutopigwa nyimbo zake kwenye redio yao alijibu "Ruby ni mtu ambaye amekuja
kujifunza alikopita ameshinda super Nyota amepata nafasi ya kuja pale kupata blasha kusaidiwa kurekodi,kajihisi yupo tayari kwamba haitaji dili zetu ndogo ndogo anaruhusiwa kuondoka.Kuna watanzania wanapenda bifu mtu akiwa na Uhuru wa kwenda mahali anaweza kwenda sina tofauti yeyote na ruby nyimbo zake na Yule na Forever nimeandika Mimi na Barnaba alisema Ruge.Aliendelea kusema alichokosea Ruby ni kuisema maneno mabaya Taasisi Clouds na Fiesta lakini Mimi binafsi niko tayari kufanya naye kazi amesema Ruge.

Alipoulizwa suala la kuwepo kwa timu kwa wasanii wa bongo Flava alijibu "Ishu ya timu kwenye muziki zilikuwepo kitambo tatizo linakuja pale kwenye athari za uteam tuliokuwa nao.Nautaka Uteam utakaoleta faida kibiashara suala ni kwamba unasaidiaje kile unachokipenda tulichofeli ni kujenga team Tanzania linapokuja suala la kimataifa.Tuangalie thamani yetu kama nchi tupo wapi,Ishu ya kuwa na team Mimi nakubali kabisa lakini ziwe kwenye Tija Kibiashara alimalizia Ruge.
SHARE HABARI HII NA WENZAKO WAIPATE
KAMA UKIHITAJI KUWEKEWA MUONEKANO MZURI(BLOG DESIGNING) WA BLOG YAKO KAMA HUU WASILIANA NA RUBEN EMMANUEL KWA NAMBA 0716528779/0755542721 KARIBU SANA

google+

linkedin

About Author
  • ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More