Siku chache baada ya Mkurugenzi wa wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Fm Ruge Mutahaba kuongea kwenye Interview aliyofanya katika radio Clouds na kusema wapo tayari kucheza tena nyimbo za Lady Jaydee kwenye kwenye kituo hicho.Msanii lady Jaydee ametoa kauli yake ikiwa kama dongo kwa wasanii wote waliokuwa wanaogopa kufanya Collabo na yeye kutohudhuria kwenye matamasha yake huku wakiamini kufanya hivyo wasanii hao wangekosa nafasi ya nyimbo zao kutochezwa kwenye radio Clouds.
HATIMAYE LADY JAYDEE AJIBU KAULI YA RUGE.
Lady Jaydee ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akisema "Kwa hiyo wale mliomba Collabo sijui feat baadae
Mkaenda kufuta Chorus zangu mtafanyaje ??.......Habari zenu buaaaaa
.....#Sawa na wao #TofautiNa Hesabu zao" alimalizia Lady Jaydee.Kauli hii ya
Lady Jaydee imekuja baada ya Mkurugenzi wa Clouds Ruge Mutahaba kusema kwamba wapo tayari kama Msanii Lady Jaydee atatoa tena Order ya nyimbo zake kuruhusu kuchezwa tena kwenye kituo cha radio cha Clouds.
About Author
ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More