Rais wa zamani wa Cuba na kiongozi wa kikomunisti Fidel Castro amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90 nchini kwake Cuba.
Akitangaza kifo chake Rais wa sasa wa Cuba mdogo wake marehemu, Raul Castro amesema Fidel Castro amefariki usiku wa saa nne na dakika 22.Fidel Castro aliiongoza Cuba kama nchi ya chama Kimoja kwa takribani miaka 50 kabla ya Raul kushika Madaraka mwaka 2008.
Mazishi ya Fidel Castro yananyika Jumamosi hii kwa mwili wake kuchomwa moto.Kutakuwepo na siku kadhaa za maombolezo ya nchi nzima.