Mwanaume mmoja raia wa Malawi aliye na virus vya Hiv amepatikana na hatia chini ya sheria ya jinsia ya nchi hiyo.Baada ya kukiri kufanya ngono na wanawake 104 bila kufichua hali yake ya kiafya "Eric Aniva" alikamatwa chini ya amri ya Rais baada ya kukiri katika mahojiano na "BBC" kwamba alishiriki ngono na zaidi ya wasichana 100 na wanawake pasipo kufichua kwamba aliugua Virusi vya ugonjwa wa Ukimwi.Wanawake wawili waliotoa ushahidi na kukiri kwamba jamaa huyo alilipwa na jamii kutekeleza "Tambiko" ambalo mwanaume hulipwa kushiriki ngono na "Wajane" waliofiwa na Waume zao.Utamaduni huu umepigwa marufuku chini ya sheria za Malawi."Aniva" pia alikiri kwamba amelipwa kushiriki ngono na wasichana wadogo na kuendelea na hilo licha ya kutambua ana virusi vya Ukimwi.Kesi hiyo imetangazwa katika vyombo vya habari vya kimataifa na imezusha mgawanyo wa hisia kuhusu ni kwa ukubwa gani Utamudi huu umetapakaa.
MWANAUME MWENYE HIV ALIYEFANYA MAPENZI NA WANAWAKE 104 MALAWI APATIKANA NA HATIA
About Author
ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More