Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Gongo la mboto Bakari Shingo anashikiliwa na polisi mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuagiza kukamatwa kwa mwenyekiti huyo baada ya kuambiwa matatizo ya bwana Bakari
Akieleza matatizo ya mwenyekiti huyo katika mkutano wa Hadhara mjumbe wa serikali ya mtaa wa Gongo la mboto amesema mwenyekiti huyo anatuhumiwa kwa makosa ya ubadhirifu wa fedha, kuchapisha risiti zisizo rasmi na kukusanya kodi
kinyume na sheria.Kuwanyima wajumbe wake kufanya vikao vya mapato na matumizi na kila akiombwa anakuwa juu na kuamua kuitisha vikao nyakati za Usiku ikidaiwa ili wake za watu waje kwa udanganyifu.
Mkuu wa Mkoa ametoa amri ya kushikiliwa mwenyekiti huyo na polisi mpaka uchunguzi utakapokamilika.