Siku chache baada ya kuachiwa video ya wakali wawili wa Bongo Flava Rich Mavoko na Diamond Platnum video ya KOKORO ni kama wanazichezea sharubu za simba mkali aliyekuwa usingizini mara baada ya video yao kutoka iliyofanyika Afrika Kusini ikionesha Wanawake waliopo kwenye Jacuzzi huku wakiwa maziwa yao wazi licha ya kupakwa rangi ya dhahabu.
Tayari baraza la Sanaa la Taifa BASATA
limehisi kuna udhalilishwaji wa wanawake kwenye video hiyo na limesema litatoa tamko iwapo litaifungia
au lah!kupitia akaunti yake ya twitter basata wameandika "katika kusimamia Maadili na udhalilishwaji wanawake
tupo thabiti video ya #kokoro ya #mavoko inapitia uhakiki taarifa itatoka".
Limeandika baraza hill kwenye akaunti yake ya Twitter.Basata walishawahi kufungia baadhi ya video za wasanii wa
Tanzania wakisema vilikuwa hazina maudhui mazuri na utamaduni wa Kitanzania.