Mchungaji mmoja wa Kanisa la Mount Zion lililopo Afrika Kusini katika mji wa Limpopo Lethebo Rabalago amezua mjadala kufuatia mtindo wake wa kuwapulizia waumini wake dawa ya MBU kama njia ya kuwapatia uponyaji katika matatizo yao.Mchungaji huyo aliyezua gumzo baada ya picha zake kusambaa akiombea watu kwa kuwa pulizia dawa ya mbu katika sehemu mbalimbali za mwili.
Kwake kila kitu anaweza kukifanya kuwa
baraka za uponyaji.Mchungaji huyo ame
sema kuwa dawa hiyo ni bidhaa tu lakini
akiiombea huweza kutoa uponyaji alimalizia mchungaji huyo.
Tayari taarifa imetoka kuwa vyombo vya usalama nchini Afrika kusini vimeanza
Uchunguzi juu ya tukio hilo la Mchungaji huyo Lethebo Rabalago.