Nahodha wa wa timu ya taifa ya Ureno na mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Christian Ronaldo ameeleza majonzi yake kufuatia msiba uliokumba ulimwengu wa soka baada ya Wachezaji na Viongozi wa klabu ya Chapecoense ya Nchini Brazil kufariki kutokana na Ajali ya Ndege.
Ronaldo ameamua kuchangia kiasi cha euro milioni 3 kwa timu hiyo kama Mchango wake wa rambirambi ambazo ni zaidi ya bilioni 9 za kitanzania kwa ajili ya kusaidia klabu hiyo na wale wote waliofikwa na msiba huo.Kwa upande mwingine klabu nyingine za Brazil zimeliomba shirikisho la soka nchini hump kuziruhusu kuichangia klabu hiyo ya Chapecoense wachezaji bure na pia
Isisushwe daraja katika kipindi cha miaka 3.Aidha waliokuwa wapinzani wao
Katika Final hiyo wameliomba shirikisho la soka barani humo,kuipa klabu ya Chapecoense kombe hilo.Kati ya wachezaji waliokuwa na klabu hiyo ni 3 tu wamesalia ambao kutokana na sababu mbalimbali hawakuwepo safarini kwenda Colombia.Mamia ya Mashabiki wamekusanyika katika Uwanja wa timu hiyo nchini Brazil kuwaombea wale wote waliofariki.Nimekusogezea picha hapa chini kuona kinachoendelea nchini Brazil: