Ndege iliyobeba Wachezaji wa timu ya soka ya Brazil yaanguka Colombia | Tino Ze Mastermind

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Ndege iliyobeba Wachezaji wa timu ya soka ya Brazil yaanguka Colombia

Ndege iliyokuwa imewabeba watu 81 wakiwemo wachezaji na maafisa wa moja ya klabu kubwa za soka nchini Brazil imeanguka ikikaribia mji wa Medelin nchini Colombia na kuua watu 76.Polisi wamesema watu 5 walinusurika lakini wengine wote waliangamia.Ndege hiyo ya kukodishwa ilikuwa safarini kutoka Brazil ikipitia Bolivia na ilikuwa imewabeba wachezaji na Maafisa wa timu ya Chapecoense.

Klabu hiyo ilikuwa imepangiwa kucheza mechi ya final ya Copa Sudamericana dhidi ya timu ya Atletico Nacional ya mji wa Medellin.Mechi ya awamu ya kwanza ya kombe hilo,la pili kwa umuhimu America Kusini ilikuwa imepangwa kuchezwa jumatano lakini sasa imesitishwa.Timu hiyo inayotoka mji wa 
Chapeco kusini mwa Brazil ilipandishwa kucheza ligi ya daraja la kwanza nchini Brazil mwaka 2014 na ilifika fainal ya kombe hill la Sudamericana kwa kuilaza San Lorenzo ya Argentina.Maafisa wa klabu hiyo ya Chapecoense wametoa taarifa wakisema "tunamuomba mungu awe na wachezaji maafisa,wanahabari na wageni wengine na watu ambao waliandamana na timu yetu.
SHARE HABARI HII NA WENZAKO WAIPATE
KAMA UKIHITAJI KUWEKEWA MUONEKANO MZURI(BLOG DESIGNING) WA BLOG YAKO KAMA HUU WASILIANA NA RUBEN EMMANUEL KWA NAMBA 0716528779/0755542721 KARIBU SANA

google+

linkedin

About Author
  • ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More