Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye amepokonywa na Serikali shamba lake lenye ukubwa wa hekta 33 kwa kile kilichoelezwa kushindwa kuliendeleza.Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi amesema kuwa serikali imefikia uamuzi huo baada ya Sumaye kushindwa kuliendeleza kama notisi ya siku 90 ilivyoeleza.
Oktoba 28 mwaka huu Rais John Magufuli alibatilisha hati ya kumiliki ardhi ya shamba namba 3074 lililopo
Mabwepande shamba hili lilikuwa na hati namba 53086 jina la mmiliki lililoandikwa katika hati ni Frankline Sumaye amesema Hapi.
SUMAYE APOKONYWA SHAMBA LAKE NA SERIKALI.
Baada ya Rais Magufuli kubatilisha hati hiyo Hapi amesema kuanzia sasa ni marufuku kwa Sumaye kujihusisha na shamba hilo."Kwa sababu hati yake imeshabatilishwa na ikibainika kufanya chochote vyombo vya dola vitachukua nafasi yake."Vyombo vya ulinzi na usalama vitakuwepo kwa ajili ya kuhakikisha kwamba shamba hili halifanyiwi shughuli zozote,isipokuwa taratibu za manispaa zitakapofanyika.
Amesema amemwagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Aron Kagurumju
"Kupima viwanja vya shamba hilo na kwamba wananchi waliokuwa na mgogoro wa shamba hilo wafikiriwe"
Amesema Hapi.Alipotafutwa kwa simu Sumaye amesema hana taarifa hizo na kwamba yupo nje ya Dar es salaam alimuomba mwandishi amweleze aliyesimamia mchakato huo baada ya kuelezwa Sumaye amesema "Unataka nieleze nini wakati umeniambia Rais Magufuli amebatilisha",Ila niseme nikirudi Dar es salaam nitalifuatilia na kuchukua hatua zinazostahili alimalizia Sumaye.Waziri mkuu huyu Mstaafu anamiliki mashamba makubwa Morogoro na Mabwepande Dar es salaam.
About Author
ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More