Rufaa ya Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema imeshindikana tena Leo baada ya upande wa jamhuri kuweka pingamizi ya kuwasilisha notisi badala ya rufaa ambapo Mbunge huyo amerudishwa rumande kwa mara nne.
Upande wa Jamhuri uliokuwa unawakilishwa na Mwanasheria Matenus J Marandu ambaye amesema wamefanya hivyo ili kuharakisha na wamekubaliana na pande zote mbili.Wakili wa Chadema Peter Kibatala amesema wameshakamilisha taratibu zote za kisheria kuhusiana na pingamizi hilo na wanasubiri pingamizi lililowekwa na upande wa serikali.
Jaji aliyekuwa anasikiliza pingamizi hilo Fatma Masengi ameelekeza upande wa serikali wawasilishe hoja zao kwa njia ya maandishi kabla ya November 30 ili aweze kutolea uamuzi December 2 mwaka huu.