Baada ya Msanii Ommy Dimpoz kutoa povu lake na kumsema Diamond kwenye interview aliyofanya akimshutumu Diamond ni kama mtu mwenye roho mbaya,mwenye wivu asiye na msaada kwa mtu.Hitmaker huyo wa ngoma ya Salome Diamond naye amemjibu Ommy kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akiandika kauli yenye Utata yenye maneno yafuatayo "Basi nilivyokuwa mshamba Nikajua mtu mwenye roho mbaya na mbinafsi Mungu ndio Humuadhibu na Kumfelisha kwa roho mbaya lake ili asifanikiwe.......Halafu mwenye roho nzuri mungu humlipa kwa kumfanya afanikiwe zaidi na zaidi.....Asa nashangaa mwenye Roho mbaya eti Mungu ndio kamfanikisha halafu maskini ya Mungu mwenye roho nzuri eti miguu juu.......Au pengine mwenyezi mungu kakosea kidogo kwenye mahesabu yake....??? hii nayo ni #Kokoro alimalizia diamond kwenye instagram yake.Lakini hakuishia hapo alitoa post nyingine kama dongo tena kwa Ommy Dimpoz akisema "Sema kugombana na Manager wako kisa eti ana demu unasikia wivu hii ni #kokoro zaidi alimalizia Diamond Platnumz kwenye Instagram yake.
BAADA YA OMMY DIMPOZ KUTOA POVU LAKE DIAMOND ATOA JIBU LA UTATA, WEMA SEPETU AINGILIA KATI UGOMVI HUO
Kufuatia majibizano hayo mtu anayedaiwa kuwa mmojawapo wa chanzo cha ugomvi kati ya Ommy Dimpoz na Diamond Madam Wema Sepetu akukaa kimya naye alijibu kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram akionesha yupo upande gani na kuandika hivi "Busara,upole,hekima.....
that's wat ur made of......I'm very very
Proud and Impressed kwakweli.......
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.....
Sasa sio mje muanze kusema sijui napick sides.......Nooo......!!!sina side
Maana na Mimi pia ni outsider tu....But
Kwa leo nimependa ulichofanya Ommy
Forever Bar....Sometimes being the
bigger person doesn't hurt ....Alimalizia the sexy lady Madam Wema Sepetu kwenye Instagram yake.
About Author
ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More