Mwanaume mmoja mkazi wa kijiji cha Ishinabulandi kata ya Samuye wilayani Shinyanga bwana Kadami Mwendagiza 34 amemuua mkewe Mwajuma Janga 29 kwa kumkaba shingo na yeye kujinyonga kwa kanga
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Muliro Muliro tukio hilo lilitokea Nov 25 mwaka huu saa 3:30 asubuhi.Alisema Mwendagiza alimuua mke wake kwa kumkaba shingo na kusababisha mauti yake kwa kukosa hewa.
Muliro alisema baada ya mwanaume huyo kumuua mkewe na yeye alijiua kwa kujinyonga kwa kanga nakujitundika katika kenchi ya chumba walimokuwa wanaishi wanandoa hao.
"Kabla ya tukio hilo wanandoa hao walikuwa na ugomvi wa familia wa mda mrefu hali iliyosababisha wanandoa hao waondoke Dar es salam walipokuwa wanaishi na kufikia kwa wazazi wa Mwanamke katika kijiji cha Ishinabulandi kujaribu kupata ufumbuzi wa mgogoro huo".
alisema kamanda Muliro.Alisema siku ya tukio wanandoa hao waliamka salama na wazazi wa Mwanamke waliwaacha nyumbani na kwenda kwenye shughuli zao za Uchumi lakini baadaye Ugomvi ulianza tena na ndipo yalipotokea madhara hayo.
Kamanda Muliro alisema maiti zote tayari zimefanyiwa uchunguzi na ndugu wamekabidhiwa waendelee na shughuli za Mazishi.Marehemu hao wameacha mtoto mmoja Ibrahim Kadami 10 ambaye ni mwanafunzi wa darasa la 3 katika shule ya Msingi Bugijibaga Mkoani Shinyanga.