Rais Mteule wa Marekani Donald Trump amemchagua Gavana wa Carolina Kusini Nikki Haley kuwa balozi mpya wa Marekani katika umoja wa Mataifa.
Tayari Trump amethibitisha bayana
nia yake ya kuwaleta watu pamoja.
Nikki Haley ambeye alimpinga Trump wakati wa kampeni za kuwania kiti
cha Urais ni Mmarekani wa pili mwenye asili ya ki_ashia,kuchukua wadhifa wa Ugavana nchini humo.
Hiyo imekuwa mojawapo ya nafasi za huu zaidi katika utawala mpya kumuendea mwanamke au mtu
asiye mweupe.