Tino Ze Mastermind: 2016

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

SALAMU ZA MWAKA MPYA 2017 ZIKUFIKIE KWAKO.

Tinozemastermind.blogspot.com

Mpendwa msomaji wetu wa Website ya
tinozemastermind.blogspot.com tunatoa shukrani zetu kwako kwa mwaka mzima kwa Ushirikiano wako kwa mwaka mzima.Tunakuahidi mwaka 2017 kukuletea Habari Kali kwa Wepesi na haraka sana bila kupitwa na chochote kuanzia Burudani, Jamii, Siasa na Michezo.


Pia unaweza kunitumia habari yoyote iliyotokea Mtaani kwenu kwenye whatsapp namba #0714082857. Pia kama una Tangazo lako au Shida yako binafsi unataka kuiweka kwenye kwenye Mtandao unaruhusiwa kunitumia muda wowote.Nitumie Story na Picha unaruhusiwa kupiga simu muda wowote.

Pia unaweza kunicheki kwenye mitandao ya Kijamii kama : 
Facebook : Tino zemastermind
Instagram : tino_zemastermind
You tube Chanel : tino Zemastermind
Twitter : tino zemastermind
Phone namba : 0714 082857

Asanteni sana wadau wote Mungu awabariki xana.Happy New Year 2017.

TALAKA NA GADNER NI 1 YA MAMBO 4 ANAYOSHUKURU LADY JAYDEE MWAKA 2016.

Msanii bora wa kike Lady Jaydee ameitaja TALAKA yake kutoka kwa aliyekuwa mume wake Gadner G Habash ni miongoni mwa mambo 4 anayoshukuru zaidi kwa mwaka 2016.
Kupitia Mtandao wake wa Instagram  Jidee ameposti vyeti vyake vya Ndoa.


Na kuandika "Funga mwaka katika vikubwa ninavyoshukuru 2016 ni kutoka cheti cha Juu na kuingia cheti cha Chini.....Bila kujali wanafikiria nini...Nilifanya hivyo kwa manufaa na furaha yangu, maisha yangu na familia yangu.Namshukuru mungu kwa kunipa nguvu kwao haikuwa kazi rahisi ukizingatia swala la kuogopa watu watakujudge vipi.Baada ya Battle ya nafasi takribani miaka 2....Naomba makofi tafadhali....Sitegemei tena kauli za nilikufanyaje sijui miaka kadha, au emoji zisizoeleweka.Utoto huooo....Mtu akimove on hana haja kufanya utoto wote huo,uki move on hujali chochote.Kwa neema ya Mungu nawaombea wote ambao hamja get over situations mbarikiwe mtoke kwenye kuwaza Past,Maisha mbona ni matamu tu ukiamua
#Kataakuwamtumwa
#Chaguakuwanafuraha
#Gutsoverfear
#Komando
#MoveonNigga.

Mkito Watoa List Ya NGOMA 5 Zilizowavutia Watu Wengi Kupitia Mtandao Huo Mwaka 2016.

Mtandao wa kuuza nyimbo za muziki Nchini Mkito.com umetoa List ya Nyimbo 5 za wasanii wa muziki nchini ambazo zimepakuliwa zaidi kupitia Mtandao huo ndani ya mwaka 2016.

Kupitia Akaunti ya twitter Mkito wameandika "tunapofunga mwaka hizi ni baadhi ya Ngoma zilizowavutia watu wengi 2016 hebu tutajie zako 5 ulizozikubali zaidi mwaka huu 2016.


Mtandao huo wa Mkito kwa sasa ni mmoja kati ya mitandao mikubwa Nchini Tanzania ambayo inategemewa na Wasanii kwa kuuza Nyimbo zao.

Magazeti Ya Leo Tanzania Disemba 31 Jumamosi #Headlines.

Nimekusogezea Kurasa za Magazeti ya Leo Tanzania Disemba 31 Jumamosi vichwa vya Habari vya Siasa Jamii na Michezo.

PICHA : Hali Ya Mwanamuziki Chid Benz Yazidi Kuwa Mbaya.

Mwanamuziki Rashid Makwilo Child Benz "CHUMA" imezidi kuwa mbaya baada ya kutoroka kwenye Nyumba ya Matibabu Sober House alipokuwa akipatiwa matibabu kutokana na kuathiriwa na Matumizi ya Dawa za Kulevya.


Kwa kadri Picha zake zinavyosambazwa kwenye Mitandao ya Kijamii inayoonyesha dhahiri kuwa Mwanamuziki huyo hali yake inazidi kuwa mbaya tofauti na alivyotoka kwenye nyumba ya Matibabu ambapo aliweza kurekodi Wimbo na Pia kutumbuiza katika Matamasha kadhaa ya Muziki.

Tayari Babu Tale aliyekuwa amejitolea kumsaidia awali alisema hawezi kumsaidia tena kwani alishafanya hivyo ikashindikana na kusema Chid Benz ni sawa na Sikio la kufa halisikii Dawa.

Licha ya kuwa inadaiwa kuwa hataki kupatiwa matibabu lakini dhahiri kuwa kwa hali yake ilivyo sasa anahitaji msaada tena wa Haraka zaidi kuweza kuyanusuru Maisha yake. Hizi hapa Picha za Mwanamuziki huyo kwa sasa :

FRANCIS CHEKA ATANGAZA RASMI KUSTAAFU NGUMI.

Bingwa wa Dunia wa ngumi za kulipwa mwenye rekodi ya kutopeza kirahisi mechi zake katika Tanzania anayekipiga uzito wa kati Francis Cheka ametangaza rasmi kuachana na Mchezo huo wa ngumi na kujielekeza kwenye Masuala ya kibiashara.


Cheka "NGUMI JIWE" mwana wa Morogoro amesema haya wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro kuhusu taarifa zilizolipotiwa na vyombo mbalimbali vya habari na kuzagaa kwenye Mitandao ya kijamii vikimhusisha na Utapeli wa kukimbia Ulingoni Disemba 25 mwaka huu jijini Dar es salaam.

Alikotakiwa kupigana na Bondia Dula Mbabe ambapo amebainisha kutofika Ulingoni siku hiyo hakukumaanisha kuhofia Pambano hilo bali ni kutokana na Promota wake Kaike Selagi kutomlipa Fedha zake zote kama walivyokubaliana ambapo amedai alipaswa kulipwa Milioni 9 lakini hadi wanamaliza kupima Uzito alikuwa amepewa milioni 3 pekee.

Akizungumzia azma ya kuachana na Ngumi Cheka amesema kwa muda mrefu amekuwa akipigana bila Mafanikio kutokana na Kudhulumiwa na Waandaaji kulipwa Tofauti na Makubaliano sambamba na Misukosuko ya Hapa na Pale anayofanyiwa na Wapinzani wake na kwamba anaamini wapo baadhi ya watu waliolenga kumshusha kwenye Ngumi badala ya Kumtengeneza Bondia mwingine mwenye uwezo wa kumpiga.

Amesema kwamba kwa sasa atajielekeza kufanya biashara zake na kuahidi ushirikiano kwenye Mchezo wa Ngumi ili kukuza na Kuendeleza Mchezo huo.

AMUUA RAFIKI YAKE.......ALA UBONGO WAKE NA SEHEMU ZA SIRI.

Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya linamshikilia mchimba dhahabu Shija Salum 38 mkazi wa Kahama Mkoani Shinyanga kwa tuhuma za kumuua rafiki yake na kula ubongo wake.


Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari aliwambia waandishi wa habari kwamba pamoja na mtuhumiwa kula ubongo wa rafiki yake aliyetambuliwa kwa jina la Shija pia alitafuna sehemu zake za siri baada ya kuzikata.

Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari tukio hilo lilitokea disemba 25 mwaka huu usiku katika kijiji cha Manyanya kata ya Makongoros wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya. "Alisema mtuhumiwa na marehemu walifika kijijini hapo wakitokea Shinyanga miezi 3 iliyopita,inasemekana wawili hao walikuwa marafiki kwani walifika wilayani Chunya kwenye Machimbo ya dhahabu yanayomilikiwa na Mfanyabiashara Teddy mwantega".

"Siku ya tukio hilo marehemu Shija alikuwa amejilaza mahali na hapo ndipo alipofika rafiki yake huyo akiwa na Panga mkononi na kumkata kwa nguvu kichwani.Baada ya hapo alimvua nguo na kuzikata sehemu za siri za marehemu na  kuzishika mkononi.Wakati akiwa na sehemu hizo za Siri mkononi alichukua Ubongo wa Marehemu na kuula kisha akatafuna zile sehemu za siri za marehemu"alisema Kamanda.

Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani baada ya Upelelezi kukamilika alisema Kamanda Kidavashari.

 

Magazeti ya Tanzania Leo Disemba 30 Ijumaa #Headlines.

Nimekusogezea kurasa za Magazeti Ya Tanzania Leo Disemba 30 Ijumaa vichwa vya habari vya Siasa Jamii Dini na Michezo.