Timu ya Simba imetwaa ubingwa wa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20 baada ya kuifunga timu ya Azam Fc kwa njia ya Penati 5_3.
Mpaka mapumziko timu hizo zilikuwa sare ya 1_1 huku goli la Simba likifungwa na Moses kitandi dk 14 na goli la Azam lilisawazishwa na Shababi Iddi dk 32 aliyeunganisha pasi ya Rajab Odas.Kipindi cha Pili timu ya Azam ilipata goli la pili kupitia Said Issa dk 56 lakini dk 5 kabla ya Mpira kumalizika Simba wakasawazisha goli hilo kwa Said
Hamis dk 86.
Mpaka Mpira unaisha matokeo yalikuwa 2_2 na dk 30 zikaongezwa ambapo matokeo yalibaki 2_2.Katika matuta "Penati" magoli ya Simba yalifungwa na
Kelvin Faru,Said Khamis, Vicent Costa, Moses kitandu na Mwakiru.
Kwa upande wa Azam Penati zilifungwa na Abas Kapombe, Rajab Odas na Adolph.