Rais wa Cuba Raul Castro aliongoza makumi kwa maelfu ya wananchi wa Cuba pamoja na viongozi wa dunia katika kuuuga mwili wa Fidel Castro.
Viongozi wa Venezuela Nicaragua na Bolivia walihudhuria.Rais Raul Castro aliongoza tukio hilo la kihistoria la kutolewa heshima za mwisho kwa kaka yake Fidel katika jiji la Santiago.
Raul Castro aliapa kuenzi misingi ya kisocialist iliyowekwa na mwana mapinduzi huyo aliyefariki dunia November 25 akiwa na miaka 90.
Alitangaza pia Cuba itapiga marufuku majengo au barabara kutumia jina la Fidel Castro kutokana na ombi kiongozi huyo.Pia alisema hakuna sanamu ya Fidel itakayowekwa Cuba.
Mbele ya mhadhara mkubwa mjini Santiago alisema Fidel Castro hakutakiwa kufanywa kama kiongozi wa madhehebu.Jivu la aliyekuwa Rais wa Cuba umezikwa katika kiunga cha makaburi mjini Santiago familia na wageni wachache walialikwa katika shughuli hiyo ya faragha iliyofanywa karibu makumbusho ya shujaa wa Cuba Jose Marti.Kumemalizika siku 6 za maombolezo ya kitaifa nchini Cuba.Baadhi ya picha nimekuwekee hapa chini ya kilichotokea :