NJEMBA MBILI JELA MIAKA 3 KWA KOSA LA UKEKETAJI. | Tino Ze Mastermind

TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS,MUSIC,VIDEO AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

Breaking News
Loading...
TANZANIA NEWS,POLITICS NEWS,CELEBRITY GOSSIP,ENTERTAINMENT NEWS AND SPORTS NEWS 24 HOURS.

NJEMBA MBILI JELA MIAKA 3 KWA KOSA LA UKEKETAJI.

Watu wawili wa vijiji vya Nyamburi na Masongo mkoani Mara wamehukumiwa kifungo cha kwenda Jela miaka 3 kila mmoja baada ya kukutwa na hatia ya kumkeketa Msichana mwenye umri wa miaka 14.


Wawili hao waliotajwa kwa Majina ya Wegesa John miaka 60 mkazi wa kijiji cha Nyamburi na Mbusiro Ketari miaka 53 kutoka kijiji cha Mosongo walihukumiwa kifungo hicho na Hakimu Mkazi Amaria Mushi baada ya kukiri kutekeleza kitendo hicho.

Mwendesha mashitaka wa Serikali Paskael Mkenyenge ameiambia mahakama  hiyo kuwa Wegesa na Mbusiro walitekeleza ukeketaji huo Disemba 15 mwaka huu na kukamatwa disemba 16. Akisoma hukumu hiyo mbele yao Hakimu Mushi alisema kitendo cha Ukeketaji ni cha Kikatili na Kinyume cha Sheria hivyo Adhabu hiyo iwe fundisho kwa wengine.

Wakiwa nje ya Mahakama hiyo wawili hao ambao walisikika wakidai "Kuwa walidanganywa kuwa Serikali Imehalalisha Ukeketaji".Watuhumiwa hao hawakuelewa kama tayari wameshahukumiwa kifungo cha Miaka 3
Jela hata walipotoka mahakamani hadi walipojikuta wakiwa chini ya Ulinzi tayari
Kwa kupelekwa Gerezani.
SHARE HABARI HII NA WENZAKO WAIPATE
KAMA UKIHITAJI KUWEKEWA MUONEKANO MZURI(BLOG DESIGNING) WA BLOG YAKO KAMA HUU WASILIANA NA RUBEN EMMANUEL KWA NAMBA 0716528779/0755542721 KARIBU SANA

google+

linkedin

About Author
  • ASANTE MSOMAJI WETU KWA KUTEMBELEA BLOG HII MAALUMU KWA HABARI MBALIMBALI, USISITE KUWASILIANA NASI KAMA UNA HABARI PICHA VIDEO MAONI NA USHAURI MATANGAZO YA BIASHARA N.K. NAMBA ZETU NI 0714082857Read More