Wananchi wa Mji wa Brazil nyumbani kwa timu ya Chapecoense iliyopoteza wachezaji wake kufuatia ajali ya ndege iliyotokea nchini Colombia walikutana kutoa heshima zao za mwisho kwa wachezaji wa timu hiyo.
Takribani watu 100000 waliingia mtaani
nusu ya watu wanaoishi kwenye mji wa Chapecoense na kuingia uwanja wa timu
hiyo unaochukua watu 200000.Mvua kubwa iliyonyesha haikuwazuia waombolezaji kushuhudia tukio hili la kusikitisha.
Miili ya watu hao ilirudishwa kwao Brazil wakati ambapo imebainika kuwa rubani wa ndege hiyo Miguel Quiroga raia wa Bolivia "alizidanganya mamlaka za Colombia kuwa ndege ilikuwa na mafuta ya kutosha kuweza kumaliza safari".Ajali
hiyo ilisababisha vifo vya watu 71.Angalia picha zaidi hapa kilichotokea: